Wednesday, July 11, 2012

ELIMU MTAANI..

Elimu ni kuweza kukua katika uelewa,hapo nikitaka wengi ama waliokusudika kufika mahala wanapopapenda,kwa namna iliyo moja hadi nyingine ikiwa ni yoyote,kwa chochote kinachoweza kutokea  kulingana na mazingira yaliyopo ama vile nikayaita hayo yenyewe mazingira ni elimu,elimu mtaani ni ‘experience’ tosha,inatosha kwa kusoma haya yaliyopo mtaani maana ndiyo mwongozo ,kwani Yule anayekosa hukosa wapi?umetaka kufundishwa shuleni ukasahau makosa,umejifunza usiyoyajua na kuacha usiyotakiwa kuyajua,hatutakiwi kutenda makosa

Mtaa kwani wa nani?hivi wengine hatupiti mitaa ile maana kuna wakabaji sana,imeitenga halisi kwa kutaka vya rahisi,leo kabeni na mkiongezeka japo siku ifike arobaini na tano,maana arobaini zinapita sana,siku zinabadilika,yale yaliyomtaani kufahamika kama si ya kihalali,ikiwa watu hawana kwa kula wala kulala mahali,siwezi kuuliza ni lini itakuwa ‘graduation’ ya elimu yetu ya mtaani,kwani kumekuwa na mafanikio,yasiyohitaji cheti.

Leo mitaa imejaa sana.tena hapa haijatofautishwa kwa vile wale ni wazee ama ni vijana,au watoto imetutaka kusoma pamoja maana kinachofanyika ni kile kimoja na haina haja ya kukosea kwa kufanya vile ilivyo tofauti na mkubwa wako,maana tofauti hiyo ni ‘experience’jaribu uone ili kufikisha taarifa katika mitaa,maana sio kuonekana tu hadi kufikirika,utakuwa ni mtu wa hivyo maana ikawa unatofautisha mtu aliye na 'certificate' na Yule asiyenacho,elimu mtaani haina mwisho,elimu mtaa haijali muda wala umri hata mzee wa miaka mia anaweza kuwa darasa la kwanza,ni kwa sababu madarasa hupanda na kushuka,leo kwako na kesho kwangu.


Tuesday, July 10, 2012

ULIMI..


Maneno hayana pa kutokea kama sio mdomoni,ilivyo maandishi kwa kuandikwa,pengine ukiwa unataka haraka kuelewa nini maana ya ulimi kabla ya kuufahamu mdomo,kile kinachotoka katika ulimi kinapita mdomoni pia,maana mdomo umejawa na yaliyo katika ndimi ni yanapita tu,

Ni  maneno ya wasanii,wasanii wachache wanaofundisha wakitaka kueleza,mimi ni mlinzi ya kuwa nalinda. na Yule anayemuongoza mlinzi yeye sijui anafanyaje..naogopa kugeuza ulimi wangu,kwani sijasema nimeshindwa kulinda.Haya hayajalambwa labda uyaone ya pembeni,

Vyovyote iwe ikataje kwa namna iliyozoea,naupenda ulimi wangu kwa uvumilivu
 wake,nikikumbuka mara ya kwanza nikipata pilipili,maana nao ulipokea ukisema haya ni mafunzo,tena elewa..asikudandanye mtu hili limeshindikana,maana ulimi unaweza kuwa umegeuka,hata usijaribu kugeuza ikiwa hautaki kusema tofauti,maana hata mpaka  sasa umedanganywa sana na kuambiwa samahani ni ulimi tu..

Unapofanya meno yako yafurahi ni pale uunapoulaza ulimi wetu,kweli hata mkafurahi wengine na wakapewe shida nyingine,maana ulimi kazi yake kuleta maneno.wacha waseme ,watasema mchana usiku watalala,akianza kumung'unya tu ujue ulimi unaelekea maala pake.
ukikaa kimya inaeleweka umekubali,asikukubalishe mtu asijue ni kwa shida ama ni kwa raha tu.

Maana meno yamefanya kazi sana,hata wakasema wasisikike,tena ukifikiri ni nini kama sio ni wewe mwenyewe umeamua,hapo unataka kusema kama unataka kusema utakatwa ulimi,sijui ili meno yasichoke na vingine tunadanganyana sana,vingine havina maana.


Monday, July 9, 2012

NASHANGAA.!


Nashangaa kuona watu wanashangaa,maana sijui kipi ni kigeni,ama mimi ni nani,wewe je?pengine tusifikiri utamu wa sukari tukasahau wa asali,wengine watasema si yale yale tu lakini ile kuandika nyingineyo yenye maana mbadala bila kujua kama kuna maana tofauti hapo hatutaelewana ,hapa nafsi zitatutoka zana baada ya kuja kushangaa kama kweli ya fulani ndiyo ya kweli,ukisahau anaendelea kuishi kwa nini tusimkataze utapeli wake,maana zaidi utaingia kwa watoto wetu hapo inakuwa ni jasusi na mtutu.hatutashangaa vifo hapo,yamkini uwepo tu.

Karibu nyumba ya pili kuna sherehe,kumbe hapo mgeni kamkaribisha mgeni,hapo mwenyeji kaingiliwa na mgeni,haya mengine ni baadhi ya furaha katika yale machache yanayokuja,pengine tusijekushangaa hata yaliyopita,hapo yatupasa kuyarudia na sijui mageni ni yapi..?zamani ndiyo watu walikuwa wanashangaa mataa kwa sababu walikuja kwa ajili hiyo,siku hizi hata vijijini kuna mataa..kila mtu anatafuta lake,kila mtu anasiri yake moyoni..kila mtu na kitu vipo hivyo kwa sababu hiyo.

Tunakuja kustaajabu haya ya musa sasa,naona tunashangaa jua kuwaka mpaka jioni,maana yawekuwa nastahili la kuzama,kaisari kama unataka nipe ila kama unaitaka chukua,maana lipi limekuwa bora kama sio la kuambiwa?angalia hayo yote ni kwa sababu ya kaisari,mwanangu angalia pengine usisahau kusali.nashangaa kuona nilitaka kuandika mengi na nimeishia hapa,hili geni sasa,hili jipya akilini pengine linatoka ama linaingia,kumbe kwa geni yastahiri..

YAACHE YAENDE..!!


Maana mengine yamekuja kama tishio,mengine yamekuja ili yakionekana yaonekane ya kileo,wanajua wachache wale wanaoitwa walevi,maana kila mtu anajiona yeye mwema,katika kuishi maisha yale mtu akaishi anavyotaka,maana hata ukahamia kaburini nahisi utasikia wachache wakinong’oneza,maana wao si hawajawahi…!!hawajui nini maana ya kuona pale,ama kufika pale,pengine yale ni mengine yaache yaende,pengine yale ni mengine waache watende,

Muda huo unapofika ndiyo unakuwa wakati wangu,maana pengine ndiyo wako sasa,kama vile tunamcheka Yule anayecheza kipindi kifupi bila ya kujua urefu ukoje,mengine ni ya lazima kuelewa pale inapotakiwa kufanikiwa,maana kila mtu na mwenzake wanataka kufanikiwa,wakiwa  na tegemezi na kwenda nayo yale waliyo nayo na kama ni maadui basi kheri waongezeke,hapo wakiwa wawili pamoja na Yule mshamba,maisha sio kuelewa sana sana ya kutaka kuelewa sana,maana hapo tutakuwa tunaelewa tu,labda kukumbuka,na wala haina haja ya kuyakumbukia wacha yaendee..

Kesho tutalia zaidi ilivyo ya leo,maana hichi cha leo tulikijua tu,pengine tumezoea sana ili kutaka kueleweka,akiyafuata  Yule mjinga na mwenzake atamcheka,hapo tutapigana na kukumbuka umoja wetu usioeleweka,kuna Yule amepata kitu na asijue nini kile zaidi ya Yule anayepata kitu na kujua nini hiki,hiki kinatumika,zaidi ya vile ikafikirika maana kwa mwengine anaweza kuwa hafikirii mmoja unapofikiria,pengine sio wengi,pengine sio mengi,haya mengine tuyaache yaende tu!!

UCHAGUZI.


Hapa isipo katika maana ya nafsi,ikawe ni kwa nini imekuwa hivyo ama ukapenda ama ukakataa,yaani kwa nini tunachagua yale yanayohitaji kuchaguliwa,maana siyo kwa vile nimechagua kwa nafsi yangu,hapa ikawe imesemeka ndiyo maana ikachagulika,maana kama hakuna kilichopo ama kufanyika kwa nini ichaguliwe iyo?
hakuna namna ya kusema tunaweza kuendelea na wakati uwazi unaonekana,tena uwazi umedhirika pale kwa  mda uliotumika,maana uwazi ni kweli,

sasa ikawe hadharani sio mahala pa wazi maana hata unayoyachagua yanakuwa mabaya,ama yakijiweka urembo ndiyo ije haja ya kuyatunukia,uzuri wa kuonekana hauongozi maana,uzuri wa moyo tokea chemichemi huonekana,maana baadaye huwa bonde kubwa kwa ajili ya watu kukata kiu zao,pengine wakashangae huko,maana kwa kujiuliza ni ile chemichemi kweli?

Hapo baadaye tumeaminiana mpaka tunakuja kuchaguana,sasa uangalie kwani  hatujachagua familia,maana utasikia aah Yule ni kiongozi wa kati,maana walishamchunguza mwanzo wakisema alipendelewa kwa kupewa,sasa aliyempa naye si alichagua,hapa unasema ilo ni sahihi kupitia nafsi, ikiwa kwa nini sijui kama itaelezeka kwa haraka,maana waliochagua hawajapata kitu kabisa.wamegoma kusema,wamegoma kufanya kazi,hii hatari na chaguzi.

Mungu anawapenda watu wake ndiyo maana ya kumtoa mwanaye yesu kristu,alijua ni kwa sababu gani anamtoa yesu,hatukujua kwa sababu gani yesu alikuja kwetu,ndiyo maana ya kufundishwa,Kesho inaweza fika matokeo ya chaguzi langu kutokea,hapo ikiwa ilifikirika kwa nini na  nafsi haina haja kuhoji kuwa ni ya nini,ni matokeo tu.ni mfano tu.

Chaguzi limelenga tukio,kama unahitaji kulijua lengo ni lazima ufikirie chaguzi zetu,maana kesho ni siku ndiyo,ikiwa jana ulichanganyana sidhani kama leo tutalewana bila ya kuchagua usahihi,lazima tufanye masahihisho,lazima tuelewe kwa nini hatukuelewa,kushindwa,kuweza kwa kuwa lolote mahala pale,ikiwa tulichagua hilo.

Saturday, July 7, 2012

MTOTO WA MJINI..


Pongezi kwenu mliowahi kufika mijini,pongezi kwenu wakulima wale wa mjini na vijijini,maana pongezi kubwa kwa watu wa vijijini,hapa sasa kuna watu wengine wa mji,hawa wanakuwa wa mahala husika,kama vile unasema raisi wa manzese nikiwa simzungumzii mtu zaidi ya umjini,maana mjini bila kujipa cheo hujafanikiwa mjini kuna maharamia wa hali za kawaida mpaka nafsi mjini hatari sana maana hata kupumzika imekuwa gharama kuuliza na sh.mia tano,kama mtu unashida ya kula tu ni kheli kurudi kijijini,maana mjini unafanya nini?zaidi utauliza soko liko wapi watu wakuchaji mia tano.

Tunasema mjini kuzuri ni kwa sababu yaweza kusiwe na kwingine kumbe hata kijijini kuna mjini yake kumbe hata kijijini kuna mjini kuna nini hapa tuelezane maana wote tumeng’ang’ania mjini,hapa kweli yapasa kujipa vyeo maana vikilenga mji uliopo pengine wengine wakajifanye mbadala kama vile mtoto huweza kujifanya mtoto  ikiwezekana akue kwanza,kama vile anakuwa anakuwa na uwezo wa kuita baba ama mama,hao wakiwa ndiyo waliomleta mjini,ukijifanya wa mjini kuna wa mjini zaidi yako,maana hao wamezaliwa na mji,pengine wametoka kijijini wakiwa na fikra za mjini basi watafanya wao wayajuayo kuhusu mji wala la kuuchafua mji unajua wewe mzazi,mtoto hachapwi kwa kuchafuka.

Mjini kuna muingiliano wa watu wengi sana  kama unaishi tegemea jirani na hawa majirani ndiyo watu wa kukuingiza mjini humo lazima upotee ingawaje utarudi mahala ulipo na kama hakuna ujuzi tambua utatumia muda mwingi sana kwa kutaka kuumaliza mji mji sio mkubwa ila watoto sasa.watoto wa mjini ni hatari sana maana kama utapenda kuwa jirani yapasa kuangalia karibu zao,na huwa wanakukaribisha kwa lugha zote vile,si wanataka kula,kwani ulisikia wapi mjini kuna mashamba?yule aliyetangulia alitangulia kuujua mji,pengine bila kutegemea kama vile Yule aliyechelewa,tuangalie vijana mjini sio pa kupapatikia,kuna watoto humu wasijetuingiza sehemu tusizotegemea.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...