Thursday, July 26, 2012

KIWANGO.

Hata usipozungumzia utaifa lakini kiwango cha maisha ya mtanzania ni kidogo sana,hapa nikiwa nazungumza na watanzania wale walio na ndoto na nchi yao,kwa pale wanapofanikisha yale wanayoyahitaji na hata ukafika wakati wa kuyafanya kukuta wengine wameshayafanya hapo tumetofautisha viwango,unaweza ukawa unajua kupumua lakini ukawa hujui kupumua vizuri,kwa vile utakapoanza kutengeneza mazingira ya undai wako,ukitaka kitakachotoka ndiyo kiwe chema,sio vile kwa sauti tu kusikia bali hata katika vile vyote vilivyo ndani ya mwili,maana vyote vikiwa na maana ya kusikia nilivyosema. 

Jua lengo lako katika lile unalololihitaji maana hapo ndiyo kiwango chako kitaonekana ,maana uwepo wako na namna ya vile unavyowaza,ndoto zina yale zinachoweza kufanya ndani yake maana yaweza kuwa unaishi ndoto za watu,unalala na kuota yale ulio yatenda tkiwa mdogo unashindwa ofautisha viwango,kumbe ilipaswa kutokea katika kiwango husika,lakini kwa Yule anayetaka kiwango kikubwa kingine yeye ni lazima atajua pale ni kupanga na kuondoka na kiwango chako,kujua nini kile ambacho ulikuwa unataka ulikuwa unasema hukijui,maana pengine hukufikiri na siyo kuona kwa kushika tu vingine  ni viwango vya watu.

Mda unalala watoto wameanza kupewa shukrani,maana ilikuwa ni wajibu wao kuwasaidia wazazi.tena baba ndiyo alikuwa anasema hii ni familia fulani tofauti na ya fulani ni kwa sababu ya viwango.
‘ukitaka kumshinda adui usimkorofishe’maana kila mtu atabaki na kiwango chake,labda usiwe na viwango vyako!

Wednesday, July 25, 2012

SI MCHEZO..

mtu bora mwenye uelewa anakuwa bora zaidi pale anapokuwa,ikiwa ameelewa tu kama alianza kukua.maana ni kumbukumbu na yastahiri kukumbuka,hilo likiwa ni chaguzi lako,pengine namna ya ulivyoelewa.ikiwa ni kucheza ama ndiyo kutafuta maisha.

 sio kila lipigwalo ni ngoma,pengine tukadhani ni king’ora,maana nyie hamsikii hata kwa tarumbeta,wamepiga sana kengele lakini waliotokeza wachache,leo tunaingia huko huko mpaka tusikike,sijui kesho ije nitakiwe kusikika,nimesema wewe kwani nafsi yako niliiunganisha na umoja wangu,hivyo kitakachopigwa yastahiri kukiitikia,maana yaweza kuwa kwenda njia ya uzima,hapo tutapenda kupigia sana,tena kwa spika zikiwa karibu maskioni,si tunacheza!!

Michezo ipo mingi sana na uzuri wake ipo duniani,basi hapo wewe chagua unataka upi,maalum kwa kuushangilia,pengine katika kushangilia ikashangilia nafsi yako pekee,na hilo ni ruksa kwani bila hivyo isingekuwepo hata hiyo moja,na kila mtu akaelewe mbili yake,na mwenye thubutu la kufika asimame na aseme,mimi nimetaka vile,sio kujaribu.maana tutashangilia huku tunaburudika,shangilia nyingine yapasa kuwa tofauti eti,yaani vile vya wachache..

Tuesday, July 24, 2012

HAPO ZAMANI..

Sio lazima kuuongelea wakati uajo bila ya uliopo,ni watu tuliopewa hali,mali na utambuzi mkubwa sana juu ya dunia hii,inapofika kipindi haujajua kuhusu hali au mali basi jaribu kuelewa maana ifikapo baadeye hiyo itasemeka ilipokuwa zamani,zamani ilikuwa ukiamshwa kutoka kulala ni kula ama uende shule,nikiwa nazungumzia vijana wazee ni vigumu hata kukumbuka enzi zao.

Tulivaa vizuri bila majina yetu ya kisasa,zamani bwana ni kama majumba ya kitasha,maana utakutamani kama vile kwa mwizi pale mlango unapokuwa hauna kitasa,tunaenda tunafikiria mbele,tunaenda tunaangalia mbele,naipenda sana hii namna ya vijana wa sasa,maana wale wazee wa zamani walitabiri mavazi yao,na kama ukifuata matakwa yao jiandae kuwa maana watu wamekuwa zamani.

Zamani kuna mengi ambayo hata hayasemekani,zamani hata sitaki kutamani maana nikikumbuka ni sawa nguvu kuirudisha imani,kuna watu wa kisasa wana akili chafu sana,hii ikiwa ni tofauti na zamani,kwani kwa kuwa na muonekano mpya na akili za zamani,ama tuseme akili za nje lakini mwili ndani,hatari sana tukilinganisha ya sasa na zamani.tutaenda kwa imani tu.ya zamani ni mengi,hapa yalikuwa kama chenji tu.

KUSUDI


Unaweza kufanya jambo bila hali yoyote,maana kutokuifikiria na hata ikikatalika mwanzo mwishoni ukikosea utasema samahani,kwa sababu unafanya bila hata ya kuuliza,ukasema haukujua kwa sababu haukusikia mahala pengine,kumbe unafanya maksudi,maana kama kosa linakujaje na mwalimu yupo katika mahala husika,Pengine mwalimu hajui kufundisha.

Unapokaa chini labda ujiulize ni kwa sababu gani unapenda,na hapo utausingizia moyo,na baadaye useme kuwa moyo wako unauma,ya kwamba haujiskii vizuri,kumbe mwanzo ulikuwa unakujiskia vizuri. kumbe haujielewi,haukujielewa ni namna gani furaha unayoitaka unaweza kuipata,yapasa kwenda mahala fulani,yapasa kuthubutu kwa kuufahamu uzuri wa ua mwanzoni,na mwishowe unaweza kuona kweli lile ni ua,lakini baadaye ni lazima kuelewa   unafanyaje na hilo ua.

Kufa ni lazima hata maana yahitaji ua  kumwagiliwa na sio kukukaukia,mapenzi yamejaza matunda yote,maana hata kama ni mgonjwa anachagua lile alipendalo na usipojielewa hutapenda,ni maana ya kutokujua asili ya mapenzi yako labda haifai kuumiza wala kuumizwa pale unapopenda,na hii haina maana viongozi kutowapenda wanawaongoza

Mengine haya ya leo unalaumu kwa kukosewa,bila kudhani ya jana wamefanyaje,maana ni yale yale tu,na kama kubadilisha basi haina maana ya kushindwa,labda kuwapa miji kwa wale wa maksudi,kama ilivyo maksudi huwa haiumi,mtu anaweza tenda vyovyote,hasara ya mwanzo yaipasa kuibeba,kwani walishaamua kufanya maksudi,Angalia kesho yako inakujaje maana mambo yanaweza kubadilika tena na kudai Pumziko la jana.

Monday, July 23, 2012

DARASA HURU....


Hapa unasema tu,sio unasema sema tu ili mradi umesema maana watakwambia umesikia wapi?hawa sio wapelelezi ni wambeya tu wa mitaani,leo atakuja na lake la kusema basi faraja kubwa kwa dunia kwa kudhani na lake litakuwa limechangia kuizungusha dunia,ni mengi san ya kuongeleka ndani ya darasa huru maana humu tutasema mbona ulisusa ukaja,siku hizi kuna masomo na ukiona hutaki katika  zetu za kihuni huni wanakutupilia mbali,sijui ndiyo kifo.maduka yameongezeka ikiwa na maana kodi imeongezeka pia,kuna jamaa wanalia sukari bei imepanda sasa mnatakaje,familia za watu zi sile? 

Darasa huru uwe mvumilivu maana hakuna viboko humoo..hakuna fimbo wala sio mwili kwa kuukaribia,ni vipigo tu vya hapa na pale,maana katika maisha tunakubali hivyo vingine vipo tena vingine vinaumiza sana hata usiwe na raha maishani mwako navyo hivyo vimo ndani ya darasa huru,maana huwezi kufundishwa kuvua na wakatI hauwezi kuvua,utafika wakati tunataka tunasema leo nimeenda mjini nimekosa hela,sasa kwa nini,maana ilipaswa kwanza,haya katika darasa huru yanapatikana endapo wakati unaruhusu hasa ukiwa unataka kusikia mwalimu anakwambia nini,labdda mwalimu hakutaka wanafunzi wajue’moja jumlisha moja ni mbili’pengine kama kuna mwingine  anafikiria ukijumlisha moja nyingine ndiyo tatu,sasa hapa kuna wale walioishia kuelewa 1+1=2,1+1+1=3,na wasioelewa 1+1=2,hapa naona wengine wameelewa namba..kweli tumetofautiana kuelewa..darasa huru litakuwa ni gumu sana..wanavyotutishia hao waliomo..!!..imesemeka..

Ngoja nimalize kidogo kwahelini maana nmeandika na kazi za nyumbani yaani ‘home work’..wahaya ni watani zangu hilo neno linawezekana kuwa la kwanza kuonekana,nilisikia mmesoma sana sasa ‘home work tu mnashindwa kuzimaliza?’..au ndiyo mnamalizia kuoga..’mshachelewa nyinyi watu wao walishakwenda’..hapo sura ikiwa na furaha kama vile ukicheza mziki wa chakacha,hata tukiwapeleka madarasani bado kwani ni kama wanacheza tu..

KAMPUNI.


Maana wao wananunulika tu,hiyo ikiwa ni kama bidhaa,tena kwa noti mbili zenye thamani moja,hii kweli ni kioja..tufanye noti moja ikawa mfano wa kununulia bidhaa moja na tena ikaja noti nyingine na namna ile ilivyo na biashara kufanyika hapo tunasema kuna uharamu,tena uharamu mkubwa sana bila kugundua maana nitapenda kuelewa wageni wanapokuja kuingia kwenye kampuni mnatoa zipi,zile za kwanza ama hizi zilizofuata,maana pengine zikija za tatu tusiwe na mashaka na za pili,maana za kwanza si zilikuwepo.

Leo ndugu zangu makampuni yanaongezeka,watu wanauza watu na sio mali,maana kama hautataka kufanya kazi katika kiwango cha chini basi kafe njaa,wewe bisha kesho ikutokee maana usiiombee..kesho watoto wetu watakuja na hasira sana maana hata tukishindwa kuwa na kampuni,nchi imegeuka kuwa kampuni,ya nini nishindwe kuwa na nchi yangu,pengine ni wewe,pengine ni mimi  endapo tunakubali ,nina mengi sana kuhusiana na hapa na kama kuna mahala zilibaki basi na sisi tugawieni,maana mbona zipo nusu nusu..au mnasemaje wateja? 

Hapa ni mengi tu jamani mmeyamezea,sijui ni baba zenu wamewaambiaa?maana bora hapa vile viboko vya mchungwa,pale mchungaji anapokuwa hajui kuchunga..haya yamekuwa mateke ya kuambiwa’aya pangeni mstari..kila mmoja anakuja hapa anapigwa teke la tumbo moja moja anaenda zake kulala'..hapa kila mtu angebaki nyumbani kwake ‘kura’ ampigie nani?ndugu zangu muda huu wanosikia wachache sana,ila itakuja kueleweka,maana  hayo yatakuwa ya ‘kodi’ itabidi tuyamalizie ndani ya kampuni..

Sunday, July 22, 2012

DANGANYA TOTO

Kweli ikifahamika kweli itaumiza,maana wakubwa wamekuwa kama watoto,na watoto wanashindwa kuelewa maana wakubwa wamedanganywa na vile walivyotakiwa kudanganyia watoto ni mchanganyiko maisha magumu mtu anajiuza nafsi kwa kidogo kitu ni chakula ndiyo tena ukibisha sana utanunua hata kavu.siku hizi si kwa wanawake tu ndiyo maana hata ikaruhusiwa ndoa za jinsia flani,maana hata hawa hawa wanaume wananunuliwa na hii sielewi sijui ikiwa kununua na kuuza ni tofauti?maana Yule anayenunua danganya toto ili akadanganye toto naye kadanganywa na muuzaji,hapo baada ya kugundua mtoto amedanganganywa kweli..

Leo tunataka barabara ili tuendeshe magari yetu pale sebureni,watoto wakijinadi kwa wazazi si kuna yale magali ya ramani?samahani watoto wenzangu wa uswahili haya yanafuata yalipoelekezwa,pengine yalikuwa machafu basi yanaenda mtoni kuoshwa,na ikiwezekana huyo muoshaji anayehitaji atapata na mengine bure,ila lazima atie saini,sasa umepewa au mumebadilishana?maana watu wanakaa vyuo miaka saba mnataka muwashibishe na makaratasi..?hakuna mtu anayependa kula cha mwenzake,ndiyo maana kila mtu ana kwake,vile vya kwake kula na watoto wake,ili wasidanganyike..

Nani huyo asiyedanganyika maana wanaodanganya wanajua,kwani ile huwa ni tabia,pengine atakaa pembeni na kujifikiria baada ya kujua ukweli,pengine inauma sana ukifikiria ulipodanganywa kitoto toto,achana na hilo imakuwaje taifa zima kudanganyika?maana hapa bila kujua matokeo ya kile tunachokishangilia,tutakufa sisi na kubaki wao,tunaweza kukubali kudanganyika kwa kusema ni ‘Shida’bila ya kujua hata kama ulizaliwa kwa shida,kama kuna mtu alizaliwa kwa raha basi huyo ndiyo anawapa shida wengine..

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...