Saturday, August 4, 2012

MAISHA YA KUTUMIKA..

Katika kutumika ni lazima kusafiri na kujua katika nafsi umeweza kufikia malengo fulani,umekuwa katika akili na yote kufanyika ikiwa kila mmoja amechukua nafasi yake,kufuta yale ya zamani pengine yanaweza kuwa mabovu,katika kufanya maisha yawe katika namna ya kutumika ni kuendelea na maisha yako katika mlengo wa maono na dhumuni ikiwa vyote sio kitu kimoja,na hapo ukafungue milango yetu ya kuelewa ili uweze kuelewa namna ya kuishi,tofauti ya vile unavyotamani.

kila maisha ya mwanadamu yana maana yake ikiwa sababu imeanza kwanza,hivyo mwanadamu anapaswa kufanya na kuingia katika mawazo ambayo yanaweza kumjenga ili yeye mwenyewe aweze kuelewa sababu yake,unaweza kuishi tofauti na kusema hiyo ni sababu moja wapo ya kuishi lakini sio ile moja ambayo kila mtu anayo ya kwake,pengine haikupaswa kuishi hivyo unavyoishi,ama ilikuwa ni chini sana na kutokana na juhudi zako umefika hapo,na hiyo ni kwa sababu ilisemwa lazima kufanya ili kusaidikika,pengine mengine yakiwa ya ziada na msaada basi unastahiri kushukuru kwa yote.

Bila kukubali katika maisha ya kutumika hapo hatutatumika,hapo hautajielewa vyema vile ulivyo kwa maana ya kutokujua uwezo wa kweli ulionao katika sababu ya kuishi humu duniani,pengine inakulazimu kujua yapasa muda mwingine kupata vile vya pembeni na hiyo ikiwa kila mtu ana asili yake ya kupata kile kilicho cha pekee kwake,pale unapotumika uangalie muda ya kuwa kuna kuharibika baada ya kukaa muda mrefu,na kama tutaharibika na kuendelea kutumika hapo utakuwa unajizika wenyewe ya maana kama wafu.Tuzitumikie nafasi zetu vile tunataka maisha yetu kuwa.

Friday, August 3, 2012

MALENGO NA MAONO.


Katika maisha unapaswa kuwa na malengo na maono,
malengo ni kujua namna gani mwanadamu unaweza kuishi,ikiwa tofauti na maono ni namna gani unaweza kuyakamilisha yale yaliyo katika namna gani unavyoweza kuishi,pengine ikiwa ni kwa nafsi moja tu ama ikawe katika ukuaji wa pamoja na ikiwa kiimani,akili na nguvu kiujumla,hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kumfanyia mwingine,labda sio maisha,pengine itakuja wakati na kusema hapa sikufanya na pale ilifanyika maana malengo yakiwa ni mengi kuliko maono.

Una muda na nafasi ya kuweza kutambua mahali ulipo zaidi ya duniani,
maana kama ni lengo basi lilifikirika,na likaonekana tena kwa mbali ndiyo huwa nzuri zaidi maana ya kufanyika kiuhakika,unaiona vyema,unajiandaa,pengine ikifahamika kabisa kwamba maisha mengine hapaswi kuishi mwanadamu umdhaniaye,pengine ukawa unaishi maisha ya watu wengine na hiyo ikiwa ni tofauti na malengo,na utofauti uaja zaidi baada ya kuonekana,ikiwa maono ni mazuri.

Unaweza kuona sana na usifanye lolote,na hivyo inapaswa kuwa na namna nyingine za kuyasukuma malengo na maono hayo kwani ukaongeza namna ya unavyofikiria ama ukafikiria hivi na sio vile ilivyofikirika,hapo binafsi kila mtu akafikiria lake maana haina ulazima sana wa upamoja endapo mmoja ametaka kufikiria lake pekee.pengine utaungana kwa mapenzi na mazingira yaliyopo,
hapo kila mtu akielezea kwa maono yake.

Wednesday, August 1, 2012

KUJUA.


Haina maana ya kujua namna itafanyika zaidi ya kama hukujua,maana kuna yale yaliyo marahisi na yaliyo magumu kiujumla,kumbe yastahiri kufanya maana yote  ni marahisi,unapoweka jambo na kufanya mambo ni wazi inatupasa kuwa tayari na kuweka akili  zetu katika namna ya kujua,kwa kutambua kwamba kila kitu  ni rahisi ya kuwa magumu ni mengi  nayo ni baada ya kushindwa,kwani gumu ni lile lililoshindikana,pale tukafanye yote,maana hakuna linaloshindikana kabla ya uwezo.

Katika Siku njema huonekana asubuhi,pengine ikawa yanachelewa sana kuiva ama namna ya kuangalia ikawa si vile katika kuitazama siku bora,pengine hapo tukafahamu namna ya asili yetu ilivyo au ni namna gani vile tunaweza kutengeneza mambo yetu,katika mengine yasiyo na nguvu za kikawaida yanaweza hata yasifikilike kwani la msingi ni lile ulilonalo mtu,katika kujifunza hapo hatujali uzoefu,maana ndiyo kwanza watu wanaamka.hata pengine hatuna haki ya kuishi masikini,maana kila mtu ameamka na lake,

Katika kujua hofu huwa inatatiza sana,hapa ndiyo huwa inatupelekea kuamini miujiza na maajabu ya dunia,na hii yote pengine ni kwa sababu hatujui,au ni kuhofia kujua maana ya kugopa maajabu,kuna namna moja ya kuweza kutembea kupitia yasiyojulikana,maana kwa kutembea kwako utayafahamu,hapo utaelewa na ikiwa umekuwa na umelijua lengo la kukuwa,yaani unataka uwe nani?uwe mkubwa sawa lakini ni kama wale watoto?..hapa ni lazima kujua wapi na namna gani tunaenda.

Tuesday, July 31, 2012

MAKOSA..


Machache yanakuwa ni ya kila mtu zaidi ya mwengine aliyonayo,maana kuna kusikia ikiwa mmoja amefanya tofauti,namna ya kusema ilivyo na kufanya huwa mbaya zaidi ya watu vile wanavyosema,ikiwa kiti cha mtu mmoja ni makosa kukaliwa na watu wawili,hapo baadaye tukaja na kuambiana ilibidi kufanya hivyo baada ya maongezi,na bila kudhani kabla mapema kama maongezi hayakuwepo.kumbe siyo lazima mmoja kuona vile walivyoona wengine,hata katika upande wako jua hayo ni ya kwako tu.

Ni makosa sana kumfundisha mtoto maswala ya kikubwa,ni makosa sana hata kumwona mtoto akifanya mambo ya kikubwa,pengine hapa tumeshindwa kuambiana ya kitoto ni yapi,na ya kikubwa ni yapi.pengine na watu hao wakafahamike bila ya heshima ya umri maana na yenyewe imeleta ukubwa,kuna wakubwa wanamambo ya kitoto na hayo ni makosa makubwa,pengine kwa upande wangu,labda na watoto waachwe watende makubwa.

Inasemeka katika makosa ni namna ya kuweza kufanikiwa,na wanofanikiwa ni wote ikiwa ni watoto na wakubwa,mafanikio hayana umri,pengine ndiyo maana mwanadamu anaweza kufanikiwa katika umri wowote,hii ikiwa kama atachelewa sana basi kuna makosa aliyafanya,pengine ni mipango tu.makosa sio ya kumfaya mtu kukata tamaa ya maisha kwani ndiyo nguzo ya kufanikiwa,hata mwanadamu asifanikiwe bila makosa,tunaweza kukosa vingi ikiwa ni pamoja na pesa,afya na yetu mahitaji mengineyo.tukubari kukosa pale inapotokea ikiwa ni nafasi pekee katika kuelekea kufanikiwa,lakini pale tunapojifunza kweli.

MACHONI..


Machoni kama watu mwishoni hawana utu..hawa si watu kabisa alisemeka hadi moyoni,hawa si watu kabisa kabisa.maana yawezekana na sisi tumezoea sana kupewa kwa nyuma,tunataka tunapotenda wema basi turudishiwe na wema,hawa watu wa machoni sio wa mafichoni ndiyo maana kuna kuonana,pengine hata kuonekana na kusikika.tenda wema achana na ya mwengine na tembea zako,pengine ikiwa imekulazimu kutokea isije kuwa imeilazimu ikutokee,sijui utaonekana wa namna gani machoni pa watu.

Umepewa kijiti peleka mbele unarudisha nyuma kufanya nini?tuachane na story za kuonekana machoni wachache wakilia moyoni,hili halitakuwa la mmoja lakini kwa kila Yule moyoni litakayemuingilia.tena ikiwa kwa vurugu maana hata moyo unaona katika namna yake,pengine ndiyo maana tunachagua ya kufanya,yupi mbaya aliyeamua kufanya mabaya au moyo wa uliyeamua kufanya mabaya?maana pengine kila mmoja wapo angejua angefanya mabaya tu.

Karibu tusogeleane maana tusikie mioyo inavyodunda,asante mama karibu yako mikono kuitizamia presha,sijui zitakuwa ni homa au maralia za taifa,kwa macho hatutaona tukisubiri hatuonani,tenda unaloliona ukisubiri usimsingizie shetani,kama ilivyo kutokutenda ni ‘kutenda’kwani kinachofanyika hapo ni maamuzi,nafsi ya mtu ndiyo inaamua.hivyo tokea machoni mpaka katika nafsi ya mtu hapo ni kasi sana,maana tunasema haya mengine tumuachie maulana.nafsi,moyo,utu vimebebwa na kitu machoni

MTAZAMO..


Naona ubadirishe namna ya kutawala pengine unaowatawala wakaelewa wanatawaliwa na nini,pengine nani maana haina haja ya kusemea gizani.nilipotizama baadhi ya matendo yake nilishtuka kwa kuona,ni kweli maovu kwa kujua mema unayotizamia wewe,pengine mimi ni wewe lakini siwezi kuwa wewe,maana inahitajika wewe kuwa mwenyewe,kwa mtazamo wangu ni kheri kila mtu akafikiria lake maana maswali yanakuja kutupa majibu ya ulipotizamia.

Ningejenga barabara mbili za juu na chini,hizo zipo sawa kwa mtizamo wangu ni kheri ungekamilisha hizi za chini kwanza,hapa si unajua unachokifanya sio kugombeza kwa mtazamo wangu ni kueleza,kwa maana pengine watasema ‘alisema’. Sisi tumepita lakini wao wanokuja patachimbika sasa ni vizazi vinavyotembea na tufikiri unapotafuta unamtafutia nani kwa  maisha ya mtanzania sio ya kulala njaa labda uwe umeathirika kimanzingira.

Hivi kesho nitajali zaidi mtazamo wangu kwa kuwa na wako tofauti,basi fikiri kutenda ukizubaa subiri kalenda,maana ya kuyaona hayaeleweki ya mwengine kuliko yako,yasiyoeleweka kusemeka kueleweka,watu na wenyewe hawaelewi mitazamo yao wanachotaka ni kile walichokuwa nacho chao.pengine jumapili njema  ni ile ya kuisemea jana,pengine tukiwa na mapenzi huku tukimsujudu maulana.namshukuru baba kwa hiyo mitazamo ya maana.

Monday, July 30, 2012

MVUTO.


Navutiwa na kuona watu wanafuraha maana ni furaha kwangu pia,inanivutia kuona watanzania wameamka na kuacha kulalama,inavutia kweli kwa kuona yale magumu angalau watu wameanza kuyafanya,hapo hata kama hayawezekani lakini kuna imani na tumai ya kuliweza japo moja,hii ni kwakuwa tumeweza kukua katika upande fulani wa maendeleo,ikiwa pamoja na vizazi kuongezeka.

Pengine inavutia sana kwa kuona watu wakijishugulisha kwa vile maisha ni magumu,maana ingalikuwa ni kula tu isingelikuwa na maana ya kuvutiwa na majengo na mambo ya mjini,ingawaje tunasema mjini kuna upatikanaji wa mahitaji kiujumla na zaidi ni haki tumevutiwa na vitu hivyo,pengine tunataka tuwe nani lazima tufanye vile vinavyotuvutia,labda ikija badaye vitarudisha fadhila ikiwa na sisi tutavutia.

Unapofanya yale ya kwako ni kufanya ngazi nyingine katika kupanda maisha yako,tunaposema maisha ni yako ya maana ukifa leo wengine watabaki ikiwa walivutiwa tofauti,ingawa ni vigumu sana kwa mwanadamu kusema kile kinachomvutia kabla ya kufanya,pengine wengine wataogopa,wakisema mbona ya kwako hukusema,haihitaji nguvu katika kuonyesha kile mtu unachopendezwa nacho ni akili na msimamo ya kuwa ni wazi kufanyika.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...

POPURAL POSTS