Friday, October 5, 2012

UWEZA

Namatumaini mu wazima kwa taarifa nilizopata chache ukiwa unahitaji kupata kitu ni katika namna ikaonekana na siyo jadi,pengine ukiwa huwezi unaweza hujui kama unaweza kuweza au uliteleza na ukashindwa kueleza ikiwa kama ni dozi umeshindwa kuzimeza,mungu ibaliki Tanzania tunaweza,karibuni kwangu kwenye meza karibuni ndani wala siyo kuigiza karibuni bandani ikiwa siyo kulipiza,mafuriko yametoka mtoni baharini kuwamaliza,karibuni sana vijana kuanzia hapa mpaka angaza.
Duniani kuna mengi hakuna ya kushangaza,kichwani kuna mengi na pengine ukiwa kilaza ,leo ikiwa kesho narudia ili isiwe kujiuliza,leo isipokuwa kesho nitakaa nisijilaumu kutokumaliza,maana hata kwa kuchungulia imeonekana unaweza,ikiwa katika mechi timu na namba zozote lakini umecheza,fikiri isiwe hali ukajihisi umependeza,isiwe ikawa mali ukasema na kujibeza.
Mawazo yako yanakuwa yako pale ulipoweza,mawazo yangu siyo yako wala hauwezi kunigeza,ukifikiri wewe pengine kimawazo  utapendeza,usipopata kiwewe mengine yapasa kuyameza,karibu nakurudisha mwanzo kwenye meza,ilisemeka karibu kumbe ulikuwa umechakaza,siyo pipi ikaeleweka kusambaza,ni utamu wa pipi ukaingia kichwani na kutandaza,irukayo juu ni mitandayo wametumia wengi kuitokomeza,Tanzania nchi huru yenye amani na kupendeza,karibu Tanzania kwa imani tunaweza.

PENZI..

Hakuna mapenzi maana imekuwa ikifungulika kama ilivo katika vifungo,leo ufunge leo ubishe maana kilichopita nikama kile kilichokuja,hakuna maana ya kuumizana kama muumizaji ameonekana kuwa na wasiwasi,na pengine asije akatakiwa tena,ikiwa nafasi zikiwa nyingi basi kuna wengi,maana wengi hawawezi,
katika maisha na maisha yao ikijumuisha na yetu unapocheka yakiwa yako,furahi umeyafahamu,kinachotakiwa ni uhuru,tena isifuatike wala kufutika,maana yataonekana mengi,na wengine kuwa wengi maana wamejaa sana.
Siwezi kukimbia wakati namna iliyopo ni katika maana ya kuiweka iwe sawa,ati fulani akawa nani ni kwa sababu ameamua,isikufanyike kusimama kwa kutaka kuvunja sifa pengine inapoeleweka kuna kuchelewa katika maumivu ili na kesho isihitajike tena,labda ikiwa inayotembea ndiyo inayokuja pia,ikiwa hakuna mbio ziliwazwa,
Penda kile unachokipenda kwani huwa inatokea,pengine ikiwa ni kutamani lakini jaribu kuzizuia tamaa maana imetambulika hivyo,usiku ukiwa mchana haina haja ya kushangaa wakina dada wakivaa uchi,maana na yenyewe yamekuwa mavazi si kosa kwani ni mapenzi pia,hakuna anayeweza kukimbia maisha yake zaidi ya Yule aliyekimbia,maana ameweza peke yake,kama aliwezeshwa umejua wewe.kesho ikija yaitwe majina mengine maana na yenyewe yamekuwa ni zama yana mpito,angalia wanaokuona,maana watasema wamekuangalia vibaya wakati unaonekana vibaya,tafuta vizuri ikiwa hujui ni yupi.

CHAGUA MOJA..

Chagua,chagua vizuri maana unaposogeza unafikiri,unafikiria vizuri ikiwa Yule anayeweza ameweza,akiwa na jinsia pengine namna yake ama iwe katika idadi,pesa sio kuishi,unaishi ikiwa unapesa,unapochagua unajua ya kuwa unataka,unapotaka sio kiraka kwani ikiwepo jua kama ulivyotaka,pengine kilitokea bahati mbaya,maana ya mmoja mwengine ikiwa ni tofauti na yako,nguvu hazimmalizi mwenye nazo zaidi ya Yule anayeziangalia maana kwa hofu isiwe kujitetea unaweza kuhofia.
Unapoona umechagua mahala na mwelekeo wa kuelekea alafu kuona hauelekei jua ulikuwa hauelekei,hakuna atakayeweza kukusaidia zaidi ya wewe mwenyewe,nguvu zako ndiyo zitakufikisha unapotaka,pengine usipofika basi jua hazikuwa ni nguvu zako,leo haitasomeka na wengi ya kuwa’ ukweli unauma’kesho usipokuja watakuja wa maana,ikiwa katika kuelewa imeeleweka ni zaidi.
Usikubari kusema basi,ikiwa walianza zamani mpaka sasa wapo,ikiwa alianza zamani mpaka sasa yupo,wewe siyo huyo bali ni Yule maaana itasemeka kwamba ulikuwapo,fikiri nyuma maana mbele kunakusubiri,angalia mbele maana sasa meza imegeuzwa,miguu ikiwa juu kichwa chini siyo tofauti,ni namna ya kufanya kichwa kiwe kama miguu,unapotembea jaribu kuangalia mbele,ikiwa sijui unaangalia wapi maana kila mtu ana yake chaguzi,usihofu yakiwa mengi maana hiyo ni moja yako.

UMAARUFU..

Katika kujulikana siyo kuhitaji sifa pengine ikiwa haijulikani namna ya kusifia,umaarufu ni katika kujumuisha yale yaliyo mazuri na mabaya,yale yaliyo na kiburi ama ikawa sio vizuri,maneno maneno si ya kupendezesha umaarufu,ikiwa kwa kumchujaji alikamua vizuri,pengine ikaeleweke ni kipi zaidi ama ni yupi ikiwa siyo kimfano maana ikiwa inahitajika kumaanika,umaarufu hauji bure bwana,umaarufu siyo kitu cha kukupelekea kule,kama mizigo yahitajika  kuhamishwa basi wawepo wazoefu na siyo maarufu.
Katika wanyama yaweza kuwa kuitwa haramu maana ikawa siyo kwa walio na hamu,kuna binadamu wengine wakitaka umaarufu wa bure,kwa kujifanya.katika yaliyo ya jana yakikumbukwa kwa hisia kali maana ya kuupoteza umaarufu,umaarufu unapozaa huamisha namna na kupeleka kwa maarufu,hii ikiwa katika matunzo na namna ya kumiliki.vingine vikiwa ni gharama,hapa ukafikiri umaarufu na siyo gharama.
Sifa za bure siyo nzuri maana kila mtu atakujua,panapokuwa hapaeleweki ijaribike kueleweka,ikiwa mwelekezaji maarufu yupo,asije maarufu wa kujiita maana kwa usiye fahamu watakwambia ndiye ‘expert’.kumbe katika tegemezi haikujulikana bora nini maana unaweza kuwa na umaarufu usiweze kununulika.

MCHANGO.

Napenda mchango wako katika kusherehekea kuwa mkubwa,pengine ili kufanikisha mahala au kitu fulani,mchango wako utanisogeza kwa kuwa umekuwa mtu muhimu sana katika maisha yangu,pengine mungu hastahiri shukrani ya kuwa ni zake,pengine isiwe katika kuchangia pumzi ukashindwa msujudu,ukitaka vile utakavyo,ukiwa huna shukrani.maana kama kilitoka kidogo haikupaswa kusemeka kama ilikuwa ni kidogo ya lakini zaidi ya kushukuru,kwangu mimi nashukuru sana maana mchango wako umenifikisha nilipo.
Unaweza kudharau kwa kuwa ni kidogo,ikiwa hujui mchango mdogo ni mkubwa haina haja ya kufanya,leo usikae ukasema unataka mchango utakao kukidhi kwa bila ya kudhani kwa wengine,maana hata kama umechangia lakini si lazima kuchangiwa,changa wewe ili ikijichanga ufanikishe malengo yako,ikifika mwisho wa siku yasije maswali ukashindwa kuelewana kwa kuchangia kidogo,sina maana ya mchango wako endapo unategemea nikuchangie,zaidi kinachohitajika ni shukrani.Shukuru pale unapochangiwa,mungu ametuchangia vingi sana,haina haja ya kutokuelewana na kuchangia kidogo.
Haikuwa na maana ya sherehe katika kufikisha lengo,haikuwa na maana ya matajiri kutoa michango,alisifika Yule maskini aliyekuwa hana na kutoa sadaka kama mchango nzuri,kesho inapokuja usifikiri kurudisha yale ya leo na kuyafanya,maana ukiwa mkubwa utachangia wadogo kufanya vitu vyao,na hiyo ni njema katika mbingu kwa kuwaacha wale watoto wadogo kwenda zao hata wasichange,huo ukiwa ni mchango wako mkubwa sana.

Monday, October 1, 2012

TUUNGANE KULETA UFAHAMU...


Wakati mwengine ikibidi haina budi.tuungane pamoja,maana unaweza pigania kuwa jinsia ya kike na wakati umepewa uume.hakuna asiye kuwa na uelewa,hakuna asiye kuwa na akili,hakuna aliye mjinga zaidi ya mwenzake,hii ikiwa katika kichwa cha mtu,na kama umekata tamaa ndiyo ukahisi na kudhani ya kuwa wanaonewa sana katika maisha NA  dunia kukuangukia,unapokuwa na moja ili kuweka mbili ni lazima kuunganisha ili kuleta maana,pengine unapodhani kama upo sahihi sana katika upande mmoja na mwengine wakati si vile ilivyo.

Maana haya mambo yapo siyo kwa sababu zako,haya mambo yana sababu zake,ya kwako yakiwa ni machache,maana pale ukaleta nguvu katika kujenga kwa kuwa maisha ni ya wote ingawa kila mtu ana ishi katika aina yake.’unapotaka kukaa na kumnyanyua aliyepo kwa matusi ni lazima utukane’ni vyema wanajamii kuyafahamu mapya yanayoleta muunganiko pamoja na amani ndani ya mda wetu, sisi wenyewe.

Kinachotakiwa ndani ya maisha yako ni mafanikio,mafanikio yasiyo nakuleta kinyume kwa mtu,pengine mwizi anaposahau kuiba na lenyewe linaweza lisichukulike kosa,hakuna kusahau mbele ya roho za watu,Yule anayepigana hajahamasishwa kwa kuambiwa bali kuona,na ingali unaendelea kukua zaidi tenda kile kitakachokuunganisha na jamii,maana unaweza kutaka kuishi tofauti na mazingira yako.

Saturday, September 29, 2012

MADHALA...


Tusidhulike tena ya kuwa  mandhali zimetengenezwa,pengine ikiwa ni mipango tangia ya mababa zetu kwani ilivyo ki enzi za zamani babu anaweza asihusike sana,vingine vikija katika namna ya kusaidia kipato,vingine vikija katika namna ya kusema haya ni maisha tu,maana ikiwa kuna kujifariji ili ieleweke kwamba hakuna madhala ndani yake.

Mengi yanayopoteza muda huwa na muda wake wa kurudi.kwani mwanzo wa kitu ndiyo kuumbika kwake ikiwa haijatokea kuwa na mwelekeo wa kuleta madhala kwani kama ni mpofu wa macho basi atatengenezewa namna ya kutokudhulika ikiwa mtu mwenyewe umejua kudhulika,mambo na vitu vinavyoendelea ni mlengo wa wewe mwenyewe,kwani ikiwa kuna kufa haustahili kukaa karibu na madhala.

Pengine yafanyike taratibu,ikiwa tunajua kila starehe ina mtu wake basi  ni kama kumpongeza mwizi anapoiba vizuri,na kama ni mlevi basi aje atuimbie kwa maneno atayozungumza,pengine ataleta radha iliyo tofauti,imekuwa ni kama  kioo kwa vile watu kwenda na kujiangalia,yaani kuweza kuongea si namna ya kuongoza wanaoongea..isije onekana kujaribu wakati kuna uwezekano.pengine tusifanye ya kuwa tunataka kujaribu.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...

POPURAL POSTS