Hapa nazungumzia nafsi ya kila mmoja,ikiwa hata wewe
leo ukaelewa iwe katika ndoa namna ya vile maisha yanavyokuwa iwe katika hali
ya kutokuwa katika ndoa na kukuta maisha yako vile vile jinsi yalivyo,maisha bado kwa wengine
yakiwa ya uadui tu,ikiwa unawaza kuanguka kamwe huwezi kuiona siku yako ya mafanikio.maana
mazuri huja baada ya kipimo chako cha kufanikiwa,pale ukaishi maisha mengi na yaliyo jaa
vingi,pale umetegemea mengi lakini hakuna katika yale uliyoyafikiria kutenda na kutokea,maana waweza
fanya mia leo na kesho kuja moja na kudhani yale mia yalikuwa ni kanuni,mazuri
yangali njiani,mazuri yangali kuja maana kama umefikiri sahihi lazima kuielewa
ile maana ya kwanza yaani sababu.
Kama yalikuja basi hongera maana pengine sijui mtu unaishi
ukifikiria nini,waweza kuota ndoto na kulazimisha kutokea,ikiwa umezani wewe ni
mkuu sana kwa nafasi uliyopo,ukijisahau kwa kuwa fikra zako ni zimekujaa wewe pekee,kumbuka hakuna
mtu anayemfikiria mwenziye katika namna mwenziye anavyomfikiria,ukiambiwa kuongea peke yako yapasa kuelewa hasa unaposikia ukidhani rahisi ama magumu yote.mazuri yangali kuja,hayo magumu ndiyo njia ya
kwenda kuzuri,ukiwa na furaha sasa jua ni yale marahisi yamewezakana,ikiwa mazuri yangali kuja.
Furaha ya mchizi ni kufurahi,pengine furaha ya mchizi ni
anaifahamu mwenyewe,ikiwa umeona mazuri siyo ya kwamba yamekuja ,angalia kesho
usijenuna na kupewa lawama,maana si furaha yako unaijua mwenyewe,anayeamini
anapata maana anakuwa ametaka akifikiri yatakayotokea,ikiwa mwanzo wa jambo basi una mwisho,wanaposema Mungu hamtupi mja wake siyo kila mtu ni mja wa Mungu,maana Mungu wa mmoja si mmoja yule wa amwaminie mwengine na pengine kesho ifikirike ili ya jana yakaonekana ni tofauti.
Mazuri yangali kuja...!!
No comments:
Post a Comment