Friday, August 17, 2012

MAISHA YAKO....

The purpose of life is not to be happy – but to matter, to be productive, to be useful, to have it make some difference that you have lived at all.
       
Leo Rosten, American teacher and humorist

Yaweza usitegemee yakuwa haijatokea katika maisha yako,usimtegemee mtu yoyote katika maisha yako hii ikiwa ni kauli ambayo inahitaji mtu kujiamini,kujipa nguvu na sio chuki ya kujitenga,kufikiri na kujua kama maisha unayoishi ni ya kwako peke yako,maana baadaye zisije kuwa lawama kwamba fulani anapenda pesa,hapo usipofikiri unataka mtu afe?maana na kweli njaa imekaba sana mtaani,watu wanapendeza,wanakunywa na kusaza lakini wana taabu mioyoni mwao,pengine ikiwa ni mapenzi ama ni namna ya maisha yalivyoandaliwa.

Katika maisha yako kuna mengi sana,itafika kipindi utasema sasa umekuwa,hata kama ulikuwa unajiona umekuwa,maana kuna wengine wakifanya maksudi na kuona hata aibu wa wakifanyacho,hata kama ikiwa sawa ni kutafuta pesa,lakini namna nyingine ni kutafuta pesa kwa ajili ya kuzikwa,naogopa kuwa Malaya wa maneno na mwisho wa siku wakaielewa wachache,kataa kupoteza muda wako,maana kwa lile lililopita liache liende,hakuna zuri moja katika dunia zaidi ya kile akionacho mtu,pengine wengine wakafikia hadi moyoni,unaweza kukutana na maneno mengi sana hata katika mitaa hiyo ni namna ya kukupanua ubongo,yaani experience,kwa vile mtoto alianza kusikia na atasema,wakubwa wakisikia huwa ni siri daima.

Pigana maisha ni magumu sana,napigana na ikiwa kwa kila namna,,pigana sana wanadamu hawana hiyana,maisha haya ya leo unaweza kuishi kesho na kusema unaishi maisha ya jana,yanakuja mengi sana mengine yatasemekana kumwachia maulana,tutaona mengi sana kwa kuwa bado sisi ni vijana,wazee wetu wametufundisha vile ilipofika,ni wakati wa kutumia kijiko kujaza pipa kipindi cha masika,utake usitake vyote vimekwekwa uvunguni sharti ya kufurahi ni kuinama.tukiwa kama wote vijana tuombeane kheri haya maisha yasije kutuendea mlama.

):-Benson G. Makaya

KUKOSA SIO TATIZO..

Tatizo ni kwangu maana hata muda bado unazidi kwenda,nimekosa leo nikitegemea kupata kesho,ikiwa kila mtu ana kipato chake,kwa upande wangu sijapata na ikiwa kwa upande wangu ulio kwako umepata basi uhaki kuisubiria ahadi yako kama vile ninavyoisubiri,matatizo ni namna ya kuweza kutafuta,maana kama hautafuti kwa nini una matatizo?hapo ndiyo utasikia wakisema lazima kuna mchawi hapa.maisha mchawi ni wewe,hakuna mlinzi mzuri wa mwili wako zaidi ya wewe mwenyewe,hivyo ukishindwa utajiletea matatizo,tena ‘matatizo’ ni kama ‘maisha’ maana yenyewe yana mazuri na mabaya.

Duniani ndiyo mahala pa kuishi,utasikia ikisemeka kwamba duniani maisha magumu sana ,sasa wapi rahisi,unapoona nyuki wanakukimbilia na wewe kimbia,kwa mfano wa kuku anapotakwa kuchinjwa siku yake inapofika,maana siku yako ikifika hapo utajua tatizo,tena yenyewe huwa hayana hodi wala kalenda labda siku fulani yapasa kupumzika ili kusherehekea,maana itakuwa imepatikana.pengine matatizo yako ikiwa kama ni raha ya mtu mwengine,wewe unacheka wengine wanalia.hapa ikiwa lazima ujue umekosa nini.

Tatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu ikiwa ameamua kuishi,wengine wanakata tamaa kwa kuona maisha magumu,kama wale wanoenda shule na kuacha,ya kuwa shule ngumu,na bila kugunndua baadaye itasemeka ni kwa sababu shule haikuenda.maisha yenyewe ni shule,matatizo hasa ndiyo yanayomfundisha mwanadamu,kuna mengine yale yanayokosekana yakaonekana kama na yenyewe ni matatizo,sasa kama yakija na yenyewe kwa matatizo yake si utakata roho kabisa?labda ikiwa ni furaha..,maana kama kile kilichokuwepo kimekuwa tatizo basi hata  kisichokuwapo haina haja ya kukisumbukia maana tutaongeza matatizo tu.

Thursday, August 16, 2012

AHADI


Kama unavyoweza kusema utarudi tena,ikiwa umeahidiana kitu ki maongezi pengine hata vitendo,au vile jana ulisema na leo imetokea basi hakika na kesho inapaswa kutegemewa yakuwa dunia ni duara,pengine Mungu angewaahidi wana wa Israeli kupitia musa wazungushwe hata pengine wangemsaliti kwa asilimia kubwa sana,maana wengine wangejifanya wanajua kurekebisha bila ya kuhofia  yatakayo haribu kwa vile kiongozi alivyo sidhani kama ahadi zinabadilika zaidi ya kutokutendeka,maana hapo utabadilishana ya moyoni,muda unayake kaa ukiwa na subira ya kile ulichoahidiwa kesho

Hakuna na kuogopa zaidi ya kuamua vile vinavyokuja bila ya ahadi maalumu huwa havidumu,pengine ikiwa ahadi inafikirika kwa siku nyingi sana,pengine uyo aliyeahidi akiwa mwongo  ndiyo vile maana ya kutokutendeka,na kama ilikuwa ni mara moja basi haina haja ya kutegemea ya pili,pengine kama Mungu angeahidi kufika katika nchi waliyoahidiwa,na baada ya kikwazo cha bahari wakadhani sio Yule mungu musa aliyemtuma kuwafikisha wanawe mahala,lakini walivuka na kufika pale,tena waliandaliwa,uliye na imani tofauti fikiri hili ni kama neno.ahadi hata kama ni tofauti lakini ziwepo uzikute upande wa kutumia iache subra yako.

Kesho ndiyo siku njema mahala hata nilipo ni zamani,kila dakika ya kufikiri inakwenda bila hata ya kudhani umeahidiwa nini,pengine ahadi yako bado hazijatoka au yapasa kuomba tena na bora kesho ije maana yale yote ya jana yanategemeana,sidhani kufika kumi bila moja iliyopo,pengine mungu amekuahidi kitu kimoja tu pengine kila mtu akamshukuru mwenyezi Mungu vyema akafanya hivyo pengine utende yanayostahiri kwa kila mmoja wetu ili usiweze kugombana kwa zawadi zitakazo kuja kwa ajili yako ikiwa zilikuwa na ahadi.

KUWA HURU..


Kuwa na uhuru kunakufanya uwe na mafanikio,yaani ukiwa na uhuru wa maamuzi na kutenda,pengine kila mtu anatenda yake,hata Yule unayemwita mwehu naye anatenda,pengine hapa ndiyo tukafikiri nakujua kuwa  palipo na mwanadamu panahitaji akili,yaani fikra zilizotimia,ikiwa inajua nini kile inachokifikiria,pengine tumekuwa na uhuru tangu mda mrefu na tumeshindwa kufanya lolote,sisi ni wapumbavu..yaani hatuna akili maana tuliyotenda ni sawa na bure,uhuru wa bure,tena ingalikuwa wanaotupa uhuru hawatukufahamu  tungalikuwa  udongo kabisa.

Sijamwona huyu wa kunitisha maana mengine aliyasema baba,ndiye aliyenipa uhuru wa kuishi hapa duniani,mengine wala hata si haba maana hata watoto wadogo wa sasa wanayo.waswahili tunasema samaki mmoja akioza wote huoza,tukisahau walikula mpaka maiti..au mtoto wa nyoka sio nyokaa..?uhuru mwengine unatia raha sana,maana unaweza ukajiona mfalme lakini ukafika muda uliopangwa ukahisi njaa,pengine wengine wanapitisha hata siku ngapi,pengine wakiwa na ufalme wao ama vile kwa ukwabela wao,huru ikiwa inahitaji kutokea maana kuna utofauti mtatu,ama mbili kubadilishana na moja au moja kubadilishana na kila moja nyenzake,kuwa huru kuelewa..

Ilipofika siku yake ilitokea,maana wale walio na mafanikio katika mambo yao wataelewa,jinsi vile namna waliweza kukumbuka mpaka kufikia hapo,uhuru hauhusiki na utumwa.ukitakiwa kuwa mtumwa basi unatakiwa utambue mafanikio yako,sasa ujue kwa kutumia akili yako,maana mwishoni tutaona matendo yako,baada ya kifo kuna maneno machache tu..kama tungalikuwa huru kufungua mbingu basi ingeeleweka kwa uchache wake.
kuwa huru katika maisha yako maana kile kilichoandaliwa kwa ajili yako kitatimia

Wednesday, August 15, 2012

MZAO..


Omba kuzaliwa lakini sio kuzaa,pengine ni wazi inahitajika kwa umri fulani kupata japo mwana,lakini ni lazima tuangalie na kizazi kilichopo,maana kama wangu angekuwa amechelewa kidogo basi ningemuombea uhamisho wa kuzaliwa mbele kidogo,kwa maana kwangu haikuwa bado.unaposikia bilabila ni ya hakuna,sasa kama vizazi vipo na inasemekana kuwa hicho kizazi kijacho kitakuwa na hasara sana,ningependa kufahamu hatari yake lakini kumbe ni ile ile namna ya kutaka kutokufanya,maana hichi kilichotabiriwa kuwa kibovu kimekuwa kizima ni kwa sababu wale wazima walikuwa wakifikiria hasara.

Ikiwa mnyama anahitaji kupata mzao mzuri ni lazima awe anakula vizuri na kuudhulia maswala ya afya,pengine wazee wa zamani ni wazi walikuwa ni watu wa ajabu sana,sishangai ngozi nyeusi kuitwa nyani,kwani unapochelewa kuingia shuleni ni viboko na wala hatuwezi kusema wewe sio mwanafunzi,kwani hata pengine baadaye itakuja na kuulizana ‘una mtoto gani,ama vile ana umri gani?’hapo ikisahaulika kama walishamfukuza darasani kwa kuchelewa.na baadaye yakitakiwa majibu kupitia kile kilichokifanyika

Hakuna mzao mbaya bila ya mtu kutokulitumikisha tumbo lake,pengine inapaswa hadi kulala lala chini ali mradi  usisikike..kama nyoka vile.maana kwa muda uliopo sio lazima ya kusema kwamba bora angetangulia fulani,maana hii au hawa wa leo wamekuja leta ubovu,hapa nikikumbuka ya kwamba mti haupewi lawama bila ya jua,maana hata lisipokuwepo litasinyaa tu,pengine ikiwa ni mzao wa mti mwema

NAMNA(2).

Katika kufanya ni kufanya yale yanayoendana na kile kinachoendana na maisha yako,ikiwa maisha yanahitaji uvumilivu wa maelfu ya muda,kuna namna ya vile unaweza kujiuliza ni namna gani unaweza kufanya  maisha yako yakaonekana na mtazamo bora ikiwa yameonekana yanatakiwa kurekebishwa,pengine ni katika mapenzi ama vile ilivyo katika hali ya kuuboresha mwili,wachache wakiwa wanafaidi kwa migongo ya wengi,na hii ikiwa wengi wetu ni hatujitambui,ingawa kila siku tunazungumza maswala ya kujitambua na bila ya kuelewa ni kujitambua katika namna ipi?

Leo imefika usikubari kuwa mzigo,pengine ikiwa utabebwa sana tena vibaya maana na mbebaji akiwa amechoka yu radhi kuutupa mzigo wenyewe,ikiwa hakuna namna ya kuweza kusema maisha ni marahisi kwa sasa,basi ni kuyapokea kwa utambuzi  wa kufanya  na kupokea kile ambacho mtu amekiamua kupitia fikra zake mwenyewe,pengine ukawa  hausikilizani kwa sababu ya kufanya kwako ni tofauti tena bila ya kujua unaweza kutoa lawama,na bila kujilaumu mwenyewe.

Hakuna Yule asiye na kitu,maana hata katika mawazo,swala ni utofauti ambao kila mtu anajitahidi katika kufikisha maisha yake mahala husika,unapotaka kufika mahala fulani hapo ni lazima utambue mahala ulipo,ikiwa na watu zingatio wanaotakiwa kujitambua ni tofauti,kawaida ya malengo huja baada ya kufanya yale unayoyatambua,hivyo ikaja wakati tumefanya tofauti hiyo ni namna ya kujitambua tofauti,pengine hata   mtu ukafanya ukaeleweka kufanya tofauti na jinsi ilivyo.

Monday, August 13, 2012

FAIDA..


Leo imekuja yakupasa kujua faida za uwepo wapo,hakuna Yule asiyeeleweka japo kwa uzuri wa uwepo huyo si mtu mwema,pengine wewe kuwa sio mtu mwema,maana kuna uadui.ni sisi wenyewe tunaofanya ya wenzetu na kutokujua kwa nini tunafanya,maana hapo ndiyo tunajua faida zetu,kuwapo ingali hakuna maana hakuwezi kuleta faida,kwa maana ya kueleweka,pengine mwengine akakwambie haueleweki,hii ikiwa mtu anataka kukuelewa yeye anavyotaka,maana kama umekuja kuielewa yangu hii haipaswi kutokuelewa faida zangu,maana si zako labda nitakunyang’anya.

Kuna faida kubwa ya kuwepo duniani na kujitambua uwepo wako,siku hizi hadi watoto wanataka shikamoo maana wakitumia faida zao kama wakubwa,sio vile kwa kuwa ukubwa ni uzoefu,biashara zipo nyingi sana za kufanya,kama unaona unapata faida ndogo thubutu kufanya njyingine,pengine ujue wapi utapata hiyo faida kubwa,pengine ni vyema ya kuwa kumekua na maendeleo,haya ya teknolojia kiujumla,maana tusipoangalia na faida zake mwishowe tutaumia.hapo tunaweza kujua kama sio kila linalotegemewa hutokea vile ilivyo,ila huanza hivyo na ndiyo faida za namna ulivyofikiri.

Leo nchi imekuwa kubwa,watu wachache wakitumia faida za nchi,maana wao kuwapora wenye nchi,mchanyiko katika matendo ndiyo uhalisia wa kutaka kujua nini zaidi,siku tutachanganyika na kihalisia tutajua faida zetu na hasara,maana mwanzo huwa hautegemeki kuhamisha msingi zaidi ya kufikiri kukua.pengine bado hujajua nini faida zako,huo ndiyo mwanzo kwani ikiwa japo kufikiri.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...