Pengine usije ukaenda mahala bila kujua hii
ikiwa kuna kuagizwa ama kwenda,na ikiwa umeenda ni lazima ujielewe kwa namna
ya kusema unaenda,maana hata ukaendelea na safari yako itaonekana si maana kwa
wale wengine,na ijulikane kuna ulazima wa kuwazungumzia na wengine ya kuwa kuna uhitaji wa kuwa pamoja,nia ya umoja hujenga thabiti yake,hujenga yale yaliyo
yake,hujenga lile lililo na thubutu
unapothubutu kufanya jambo si kuwa na akili Fulani,si kupima uwezo Fulani,na ingali kuwa hivyo hata usishindane,na iwapo dawa ya Yule mbishi ni kutaka kuona kama imejulikana vipi,hapa akiwamo au hata asipokuwapo ueleweka wake unamfanya awe hivyo kwani muda tukiungalia huwaisha yale yaliyokuwa na thubutu la kweli,mateso na pilika za maisha zinafanya kutokusikia kwamba pengine fulani alisema nini,pale tunaposema pombe ni mbaya tunathubutu na tunaona,tunaposema simba ni mkali hata kwa picha anajionyesha na thubutu yake ni endapo anakutana na mwanadamu,hapa katika simba ni sawa na katika maisha,maisha yanaralua kisiri ya kutokusema kwamba nimeralua pale,hii ikiwa imerudiwa,nia na thabiti ya mtu haitakiwi kurudiwa zaidi ya kufanya,kufanya na kueleweka kama ilivyo,Ikitokea basi ifanyike katika uthabiti wake.
Pengine unataka kueleweka tofauti,pengine unataka
kujulikana tofauti,nia na thabiti yako ikatuthibitishie,ule uthabiti unapothibitika ndiyo huonyesha asili ya
tendo,maana itakuwa imetendeka kwa nia isiyojalikana kama ni njema ama la,hiyo
tukaiacha kwa mtendaji kutokana na akili zake,unapokuwa majumbani na kukuta unatukanwa na mkubwa wako sio jambo la kusema nani kamfundisha mwenzake,maana hata matendo mengine yanaingia bila kueleweka ndani ya eneo husika na yakitaka kuonyesha ni matatizo.
Hasara ya utambuzi si kama ile apatayo mfanya
biashara maana hapa hata nia ziko tofauti,wala kutambua inakuwa ni vigumu,hata kama akili ya mwanzo ni kufika
katika mlengo Fulani,lakini nia ya mtu itaonekana na thabiti yake,tena usichelewe ukaseme ni bahati mbaya,kwani utakuwa umenuia huko,na baadaye kuja kusema kwani
hakuona!!mengine yasipase kumwachia mungu,mengine ni yako hata haina haja
kuyaweka chini ya uvungu,utaficha yaliyo na maana,utaficha visivyo na
uelewa,hapa hutaelewa na hutamaanika,ukifanya leo nia yako iwe
mbele,ufanye leo kwa kutokuogopa yanayotokea,kwa
kuthibitisha unayafikia na utafika.
No comments:
Post a Comment