Tuesday, May 29, 2012

NIA NA THABITI YAKO MWENYEWE


Pengine usije ukaenda mahala bila kujua hii ikiwa kuna kuagizwa ama kwenda,na ikiwa umeenda ni lazima ujielewe kwa namna ya kusema unaenda,maana hata ukaendelea na safari yako itaonekana si maana kwa wale wengine,na ijulikane kuna ulazima wa kuwazungumzia na wengine ya kuwa kuna uhitaji wa kuwa pamoja,nia ya umoja hujenga thabiti yake,hujenga yale yaliyo yake,hujenga lile lililo na thubutu

unapothubutu kufanya jambo  si kuwa na akili Fulani,si kupima uwezo Fulani,na ingali kuwa hivyo hata usishindane,na iwapo dawa ya Yule mbishi ni kutaka kuona kama imejulikana vipi,hapa akiwamo au hata asipokuwapo ueleweka wake unamfanya awe hivyo kwani muda tukiungalia huwaisha yale yaliyokuwa na thubutu la kweli,mateso na pilika za maisha zinafanya kutokusikia kwamba pengine fulani alisema nini,pale tunaposema pombe ni mbaya tunathubutu na tunaona,tunaposema simba ni mkali hata kwa picha anajionyesha na thubutu yake ni endapo anakutana na mwanadamu,hapa katika simba ni sawa na katika maisha,maisha yanaralua kisiri ya kutokusema kwamba nimeralua pale,hii ikiwa imerudiwa,nia na thabiti ya mtu haitakiwi kurudiwa zaidi ya kufanya,kufanya na kueleweka kama ilivyo,Ikitokea basi ifanyike katika uthabiti wake.

Pengine unataka kueleweka tofauti,pengine unataka kujulikana tofauti,nia na thabiti yako ikatuthibitishie,ule uthabiti unapothibitika ndiyo huonyesha asili ya tendo,maana itakuwa imetendeka kwa nia isiyojalikana kama ni njema ama la,hiyo tukaiacha kwa mtendaji kutokana na akili zake,unapokuwa majumbani na kukuta unatukanwa na mkubwa wako sio jambo la kusema nani kamfundisha mwenzake,maana hata matendo mengine yanaingia bila kueleweka ndani ya eneo husika na yakitaka kuonyesha ni matatizo.

Hasara ya utambuzi si kama ile apatayo mfanya biashara maana hapa hata nia ziko tofauti,wala kutambua inakuwa ni vigumu,hata kama akili ya mwanzo ni kufika katika mlengo Fulani,lakini nia ya mtu itaonekana na thabiti yake,tena usichelewe ukaseme ni bahati mbaya,kwani utakuwa umenuia huko,na baadaye kuja kusema kwani hakuona!!mengine yasipase kumwachia mungu,mengine ni yako hata haina haja kuyaweka chini ya uvungu,utaficha yaliyo na maana,utaficha visivyo na uelewa,hapa hutaelewa na hutamaanika,ukifanya leo nia yako iwe mbele,ufanye leo kwa kutokuogopa yanayotokea,kwa kuthibitisha unayafikia  na utafika.


No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...