Wale wazuri wamefanya yao,tena ni mengi na mpaka yakawa
mazuri bora,pengine walitumia ujuzi wao na katika
maisha kitu ujuzi sio kitu kusikia,sio kitu kusema wala kufanya katika
wakati wowote wa muhitaji yaani ni mtu kuelewa
kujua na kuthamini kinachoendelea kutokana na muda,haina haja ya kutafuta ujuzi ikiwa kazi unayo,kuishi ni kufanya kazi ama shughuri ambapo unatoka ujuzi,sasa ukifikiri unaishije ndiyo utajua ujuzi ni nini maana unatakiwa kutoka mahala Fulani unapopaona,kuishi
vigumu sio taabu ni kupenda ni kama huwezi kuoa ikiwa unaishi vigumu,na kama una
uthibitisho wa ugumu ulionao hapo itakuwa haukupata mafundisho yangeyokuzoesha kufanya hata usichokipenda.
Kusudi halina sababu ya kwanini ilete maana yenyewe,ingawa hatuwezi kufanya
kitu bila kusudi,kusudi sio sababu ama mazoea kusudi ikiwa ni dhumuni,na hata tusifanye mambo ya
sababu maana tumejawa na sababu nyingi sana katika kila tukifanyacho,lakini
kusudi huwa linatimiza nia,ni kueleweka kwa kutimiza dhumuni lililotokana na uzoefu,kujua tena ni kuijua sababu iliyokosewa mwanzo,sasa ikiwa ni kwa sababu ipi ndiyo
pale tutauliza dhumuni la kila mmoja ili tuonyweshe uzoefu.
Kuna uzoefu mwingine haufai kuuzoea,hasa ule ambao hauupendi
wewe mwenywe kwani ndiyo utakuwa ni uzoefu wako baadaye unapoendelea,utakuwa umezoea hivyo kama ni
kupenda au kutokupenda,pengine unataka uzoeane,uwe na umoja uijenge nchi
pamoja maana hata ukibisha wazoefu watazitafuta sababu na kufanya yao bila ya kuuliza,umezoea kufanya nini hata ujiulize
basi na kama umezoea hivyo na haujaambiwa ni vizuri basi usubiri majibu,ulimwengu hutoa ushindi,Ushindi wako upo mikononi Mwako uko mahala pale Umezoa.
No comments:
Post a Comment