Tuesday, May 29, 2012

ACHIA


Sio ngazi tu ndiyo ikatufanye hata kufikia,pengine kwa urefu wetu huu na mbio za kubahatisha kwa mwili kuujengea,yamekuwa makubwa mpaka tunashindwa hata kusalimiana,cha ajabu mara zote hukosekana kama mmoja hajaona hivyo,kile alichonacho wewe ndicho hicho yakupasa ukifanye,maisha ni mapenzi,maisha sio kupendana kati ya mwanamke na mwanamme maana wengine hapa huwa na sababu zao,pengine wakitaka lifti ili kujaribu kuona kilichopo,au kilichopaswa kuwepo kwani taamaa ilikuja kwanza,
Leo imetufanya kuogopa,leo tumekuwa waoga ambao tusiotaka kurudi nyuma,kumbe nyingine nazo ni nguvu,yaani bila kazi yeyote na akili ikaamua jambo,ikafanya yale inayoyafahamu na kuweka msisitizo juu ya usahihi,unaweza kushangaa kwa nini mtu anakojoa barabarani na ukamwona hana akili kumbe ndiyo mahala alipozoea akiwa katika mazingira yake,huyo ndiyo halisi kwani kubana kupo wapi?yule akijikijolea tunasema hapa ilizidi na kusababisha hatari tukisahau kwa nini haikuwa hivyo mwanzo,kwa nini imekuwa hivi sasa,kwa nini haikuwa vile sasa,hapa majibu tukiwa tunataka yatoke kwa wakati huu tuliopo,tukilazimisha masaa kukimbia bila kujua  machache tuliyoyaacha kwa leo,tena yapi tunategema kuyaacha,wapi  tunategemea yakawe yameachwa pengine ikiwa si ruksa na yenyewe kupita.

Badaye yake huwa inafahamika sana,badaye yake huwa ni nzuri sana,maana ni ushindi anaoutengeneza mwanadamu na majibu yakiwapo,pale tunapohakikisha na kukuta ni ukweli inapasa tusitizamie pembeni,tuangalie tujue pale palipo na nyuma iangaliwe na mbele yake tena,pengine ndiyo usahihi ulipo.kuachia ni kutaka kujua,ni kutaka  kuthibitisha,ni kutokujua,ni kutaka kufanya kujua,haya yatatokea pale tu yatakapoeleweka

Kama tunapendwa na kuitwa wana,baba na mama,Yule mzazi naye akaitwe pia,ikiwa wao wameachia,wamefanya jambo la kuweza jambo,ili kujulikana inayoeleweka  maana zaweza kuachwa nyingi,kwa mwaka zikawa zimejaa mbovu mbovu tu.Hapo ujue wenyewe wamekaribia kuachia,si nguvu nazo zilikuwa zinatumika nyingi!!uwezo pengine hata mashine,maana kwa kawaida isiyokuwa na milolongo ya kueleweka hapo ni kujua tu,
mahala pengine ni pachafu tupasafishe kidogo,hapo tushindwe kwenda hata na wazazi wetu,mahala pengine ni pachafu sana.

Watu hawa hawa tunaojumuisha,ni watu hawa hawa wanaotunukishwa,ni watu hawa hawa wanaotunukisha,leo na kesho tusipeane zawadi kwa vizuri vile vichache vinavyotukia maana si sisi,ni vyenyewe vinajileta,tuviache hapo mahali salama,tuwaachie hao..tuwaachie hao waende kwao,tuwaachie hao waende zao.
tuachie nafsi zetu tutende yetu

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...