Endapo tulizaliwa wanadamu kunakuwa na urahisi Fulani wa
kuweza kuelewana,hapa hata ule uwezo wa kuelewa zikajulikana kama ni
nguvu,tusijali zilizopotea kwani zinazokuja ndiyo tunazoziombea,maisha ya
mwanadamu sio ya kulalamika zaidi ya furaha,pale tulipoambiwa tajiri kwa tundu
la sindano na ngamia sio pale tulipotupia nguvu zetu,yaweza kuwa ni hapo lakini
utambuzi usio kuwa na uwezo unaweza kufanya yale mengine kuwa mengine,hapo watu
wakiwa wamechoka,hawataki yale magumu na kutaka mepesi,wakiamini kuweza kwa
hali ya kawaida wakiamini kuweza kwa kusema ilikuwa rahisi bila ya kutumia
nguvu zako,kile kinachoisha kimetumika,yanapokuwapo maneno ni lazima
tuseme,
Yanapokuwapo maumbo ni lazima tuyaunganishe,maaana kutimilika kuwa moja
si sawa na nusu inayoelea,hapa tukiunganisha nguvu zetu ingawa sio lazima zangu
na zako ama za Yule bali zako,zangu na mwengine yeyote,haujafika wakati wa
kulalama wakati bado hakuna wa kumlalamikia,maana kama ni kwa mungu huku ndiko
tunapoelekea,tunapompa lawama Yule aliyezoea tutaweza kuonekana wajinga wenyewe
maana hapo tunahaki ya kuulizana kwani nguvu nyingine ziko wapi?ama hatuna na
kama ni hiyo ieleweke hata kwa kusema,isemeke ikiwa inahitaji msaada maana
inaupungufu wa nguvu
Pumziko la mtu anayetafuta ni nguvu kwa mmoja aliyelala,hapa
tusilale,hapa hakuna kulala maana wakati ndiyo huu,muda wakuupoteza ulipita na
kubaki wa kutumia nguvu,tumelishwa sana na wakubwa zetu wakiwa wazazi pamoja na
ndugu baki hiyo yote ikiwa ni kutaka kuonyesha nguvu,,hakika misemo ipo lakini
si kwa mwanadamu ikaonekana kwamba hapa au pale alishindwa nguvu,kwani maana ya
hakifai ni kile kilichoachwa jana,hakikufahamika kama kipo ama kilifahamika na
nguvu hazikuwepo,
Tusiwakaribishe wale wengine wasio na uwezo wa kufikiri,wao
nguvu zao hutumia kwa utofauti na wenye akili,wao nguvu zao hutumia ipasavyo ya
kuwa ni tofauti na sisi,wa kuchekwa hakuna maana wote hatujafanya,wote bado
hatujatumia nguvu zetu,kama tumetumia embu tuambiane ni mahara gani,yaweza kuwa
zilitumika bure na umekuja wakati ni ieleweke sasa,kipindi cha kupita hakifai
kupita tena,kipindi kinachokuja ndiyo kile tunachokisubiri,Yule anayeandaa
nguvu kwa ajili ya jana hataki la leo,ingawaje na lenyewe lilibaki tokea jana
hiyo,ni kama mpiga picha hutumia nguvu zake ili apate kula,hutembea pengine
asipokuwa na ofisi na hiyo ni kudhihirisha maana ya nguvu,akirudi aseme
amechoka na mwingine akaulize kwa nini maana yaweza kuwa alitumia nguvu ndogo
katika kufikiri iliyompelekea kutumia nguvu kubwa katika kutembea,labda tuandae
mazingira kwanza,tuyainue,tujiinue.
Onyesha nguvu zako tokea moyoni,onyesha kwa kile ukifanyacho
tangia usoni..!!
No comments:
Post a Comment