Tuesday, May 29, 2012

AMANI


Maana pengine tukaelewe kama ni imani,ikiwa ni kwa ufahamu wa mtu,pengine tukahisiane vibaya,hapo tukiwa hatujajuana,matukio mengine ni  mambo,matukio  mengine ni maswala ya kawaida,pengine sisi ni wa kina nani,pengine haina maana  ya kuwa na imani wakti wewe si mtu wa amani,amani huja pale mwenzake asimfikilie Yule mwizi,pengine mlevi hii ikiwa mmoja amejiweka mungu sasa,au hata kuonekana.sasa kama ikaja na mwignine  akawa mungu si itakuwa balaa,maana hapa wasomaji watakoma,lakini ni amani inayofanya tuwe na imani,imani yangu imeniweka ,tutavutana kwingi sana,hii ikiwa ni kutaka kueleweshana,na hapa ikiwa tutafikiria pesa basi vyote anaweza akapewa mwingine,maana kama ulikuwa na amani ikakuletea imani na imani yako ndiyo hiyo uliyonayo sasa hivi basi mshukuru mungu wako,maana amekuweka huru na Baraka mpaka sasa.

Mimi ningekuwepo zamani ningewaambia kitu,lakini kuna hichi cha sasa hichi ambacho wote tunakiona,tusifanye ije baadaye watuhadhithie,ya kwamba kama hatukuwepo vile,yaani tukatafuta bila misingi,hata tusione wala kujua nini maana ya jambo Fulani,pengine watu wengine wanacheka wakiwa hata na hasira,hii sikatai kwani mimi sio wote,ukiwa wa kuwa mmoja haujengi ukimya wa maana ya maisha ya mwanadamu,hapa tunazungumzia ukiwa zaidi,tumepoteza vingi na kila mmoja anakikumbuka chake,cha mwenzako kizuri ni kile cha mwingine kimebaki kidogo,maana hata tusingepishana tusingejua mengine,mengine kuyafahamu yakupasa kuwa na imani yenye kuleta amani,tusifanye vita kwa kujua tunakwenda mbinguni,kwani tunapoenda kwa watu bila taarifa tunajua kama wamepika chakula gani?hapa lazima tuwe na mazoea,lakini mazoea haya kuna yale ya utofauti,pengine ni mazuri tuseme.kama mkubwa anapokuwa na kwake anakuwa na amani sana,hili nimesema mimi,kwa  Yule asiye na amani basi hata akizaa mtoto ataamini ni wa Fulani,maani ile imekuja katika imani,yaani yeye akaamini hivyo

Amani ya moyo ni nzuri,hivyo ni kwa sababu ninayo,chako jipe,kama vile ilivyo katika imani,ninaamini kupitia amani hakuna kitakachonishinda mimi,hapa ukibisha basi utakuwa unahitaji kuelekezwa,mengi tu mazuri lakini lingine sio zaidi ya lenza.itafika kipindi tutaanza kutangaza makanisa katika vyombo vya habari,hapa imani itakuwa zaidi na amani itapotea,pengine lile kanisa fulani  la pale chini ni la jamaa Fulani hatumjui alafu haya mengine yakwetu,si ushindani na tunataka!!lazzima vita ije,pale tukiwa tunaamini huyu ni adui yetu lakini ingawa ni mwanadamu mwenzangu.hapa tutapoteza vingi hata vile tulivyovipenda kuliko binadamu wenzetu,amani ikipotea hakuna kinachoeleweka,maana lengo zuri la kuelewa kitu ni kuishi na hicho kitu,hakuna kuishi katika vita kwa ni tokeo lake kuu ni kifo,tulete amani sasa,kama ni nyeupe na inasema sasa si tukae chini na kuelezana,mambo ya msingi yapo mengi tu,hatuwezi kuyafanya bila amani maishani.

AMANI MWONGOZO WA IMANI MAISHANI..

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...