Wednesday, December 12, 2012
Makaya's Forum: NIA NA THABITI YAKO MWENYEWE
Makaya's Forum: NIA NA THABITI YAKO MWENYEWE: Pengine tusije tukaenda madukani tukasema ni akili zetu,hii ikiwa kuna kuagizwa ama kwenda,na ikiwa tumeenda ni lazima kujielewa kwa ...
Makaya's Forum: KIWANGO..
Makaya's Forum: KIWANGO..: Hata tusipozungumzia utaifa lakini kiwango cha maisha ya mtanzania ni kidogo sana,hapa nikiwa nazungumza na watanzania wale walio na nd...
Makaya's Forum: TENDA WEMA NENDA ZAKO..
Makaya's Forum: TENDA WEMA NENDA ZAKO..: Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kucheka,maana swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya kuhudhu...
Monday, December 3, 2012
Makaya's Forum: DUNIA YA FURAHA..
Makaya's Forum: DUNIA YA FURAHA..: Katika malengo yanayomfanya mwanadamu kuweza kuishi pengine ikiwa ni kwa muda fulani ama ki namna ilivyo kwa mtu akataka furaha iliyo...
Friday, November 30, 2012
KUMBUKUMBU..
Ni miaka mitano tangu umetutoka,Tutazidi kukuombea Baba,japo
haupo karibu Nasi kimwili lakini daima upo katika nafsi zetu,jina lako lieendelee
na likawe jema mbinguni,kumbukumbu zako vichwani mwetu hazitaweza kuisha kamwe katika maisha
haya ya uhai,tunaomba na tutazidi kuomba kwa upendo uliotuachia.
umekuwa ni pengo kubwa kwetu,ulikuwa chuma kisichochakaa bali
kuvunjika katika mipango ya mungu,nafsini tunakupenda sana,wake,watoto,wajukuu zako,wadogo na ndugu zako wakiwapo marafiki,majirani Pamoja na
jamaa.
Mungu ilaze roho ya marehemu baba Col G.K Makaya,mahala pema
'AMIN'
Thursday, November 29, 2012
Makaya's Forum: ONA MATATIZO YAKO MADOGO...
Makaya's Forum: ONA MATATIZO YAKO MADOGO...: Nafahamu kwamba katika maisha ya kila siku hayakosekani mambo ya kuumiza. Sina shaka kuugua, kufiwa, kukosa chakula, kusalitiwa katika map...
AINA NNE ZA WATU...
NI imani yangu kuwa, si wote wanafahamu kwa undani aina nne za watu
katika ulimwengu wa mafanikio, jambo ambalo naamini linachangia kwa kiasi
kikubwa kuwafanya hawa wafanikiwe kimaisha na wengine wasifanikiwe kabisa.
Kwenye ulimwengu wa mafanikio binadamu wamegawanyika katika makundi manne ambayo ni WATENDA USAHIHI, WANAOLIDHIKA, WANAOTAKA KUPENDWA NA WASHINDI. Naomba tufuatane katika kuangali kwa undani aina hizi za watu ili kuanzia leo kila mtu afahamu yupo kundi gani.
WATENDA USAHIHI:
Ni vema mambo matatu ya mwanzo yakaongozwa na la nne yaani USHINDI. Kwa maana hiyo kila mmoja wetu lazima awe mtu ambaye anatamani sana kufanikiwa katika maisha yake ya kila siku. Watu wote wakiwa na nia hii wataweza kuyapita makundi mengine matatu kwa uangalizi mkubwa.Hawatakubali wawe makini wasifikie malengo, hawataacha kujaribu bahati kwenye mambo ambayo akili zinaona ni magumu, hawataridhishwa na mafanikio au hali walizonazo na hawatakubali kutumika kama kuwafurahisha watu bali kila kitu watafanya kwa kiasi kwa lengo la kufika katika mafanikio sahihi.
Haya dunia yako, chaguo ni lako.

Ni watu ambao katika maisha yao huwa hawataki
kukosea au kuonekana wayafanyayo si sahihi. Watu wa aina hii huwa ni wagumu
sana kufanya jambo ambalo akili zao hazihakiki kuwa litamalizika kwa mafanikio.Kikwazo
kikubwa kwa watu wa aina hii mara nyingi ni kusitasita katika kuamua. Ni watu
wa kuogopa macho ya watu hasa suala la kushindwa kutimiza malengo linapowajia
akilini. Kinachowaogopesha zaidi watu wa kundi hili ni kuabika mbele za watu
jambo fulani likiwaharibikia.
WANAORIDHIKA:
WANAORIDHIKA:
Kundi jingine la watu katika ulimwengu wa
mafanikio ni wale wanaoridhishwa na hali zao na kwamba hawahitaji mabadiliko ya
aina yoyote kwenye maisha yao. “Ndugu yangu, hali hii tumeizoea, mwaka wa nne.”
Wamezoea maisha magumu.Hata hivyo, wapo wanaozoea kazi na majukumu yao ya kila
siku kiasi kwamba hawataki kubadilika, hawapendi kuongezeka zaidi ya hapo
walipo. Utakuta uwezo wa mfanyakazi alioanza nao miaka 7 iliyopita ni huohuo
mpaka leo. Wafanyakazi wengine wanaweza kuajiriwa nyuma yake wakajitahidi
kusoma, kujifunza kazi na kupanda vyeo na kumwacha mridhikaji yuko palepale.
Kundi la wanaoridhika.
WANAOTAKA KUPENDWA:
WANAOTAKA KUPENDWA:
Kuna watu katika maisha yao wanataka
kumfurahisha kila mtu kwa lengo la kuvuta upendo wa wanadamu wenzao. Utakuta
maisha yao yote ni kuwatumikia wengine kutoa fedha za maendeleo kwa kumsaidia
huyu na yule kwa malipo ya kupendwa na jamii.Ni wazi kuwa watu wanaoishi katika
kundi hili hawawezi kufanikiwa kwa sababu kipato chao kingi hukitumia katika
kuwafanya watu wengine wafurahi na si kusukuma mbele maisha yao ya kila siku.
WASHINDI:
WASHINDI:
Kundi la mwisho la watu ni wale ambao
katika maisha yao ya kila siku hupenda kufika kwenye kilele cha mambo yote
wanayofanya. Hutamani kufanikiwa zaidi na zaidi, hawakubali jambo liwashinde,
kila walichokusudia kukifanya huhakikisha kwamba wanakabiliana na changamoto
zote na mwisho wa safari kupata ushindi.
Baada ya kuangalia hayo, ni vema kujiuliza; Je ni sahihi kutokuwa makini katika mambo yako ama kuridhika na mafanikio uliyoyapata? Inawezekana kweli mtu akaacha kusaidia wenzake kwa hofu ya kuwa katika kundi la tatu? Jibu ni hili:
Baada ya kuangalia hayo, ni vema kujiuliza; Je ni sahihi kutokuwa makini katika mambo yako ama kuridhika na mafanikio uliyoyapata? Inawezekana kweli mtu akaacha kusaidia wenzake kwa hofu ya kuwa katika kundi la tatu? Jibu ni hili:
Ni vema mambo matatu ya mwanzo yakaongozwa na la nne yaani USHINDI. Kwa maana hiyo kila mmoja wetu lazima awe mtu ambaye anatamani sana kufanikiwa katika maisha yake ya kila siku. Watu wote wakiwa na nia hii wataweza kuyapita makundi mengine matatu kwa uangalizi mkubwa.Hawatakubali wawe makini wasifikie malengo, hawataacha kujaribu bahati kwenye mambo ambayo akili zinaona ni magumu, hawataridhishwa na mafanikio au hali walizonazo na hawatakubali kutumika kama kuwafurahisha watu bali kila kitu watafanya kwa kiasi kwa lengo la kufika katika mafanikio sahihi.
Haya dunia yako, chaguo ni lako.
Tuesday, November 27, 2012
KWA NINI KUACHANA?
Matatizo yanayochangia watu kuachana
yako mengi, ambayo mtu unaweza kujaza vitabu kuyaelezea, lakini uchunguzi
unaonesha kuwa wapenzi huachana kutokana na udhaifu wa sababu zilizowasababisha
kupendana. Kwa mfano wapenzi ambao wakati wa kupendana kwao walitamaniana kwa
maumbo, sura, mvuto wa kingono na pesa huwa katika hatari ya kuachana baada ya
vitu vilivyowasukuma kupendana kupoteza mvuto.
Hakuna asiyefahamu kuwa watu hubadilika tabia, umbo, sura, hufirisika na hata kutovutia tena! Hivyo mtu anapopenda kwa sababu hizo, ukomo wake huwa ni baada ya alichopenda kuondoka. Ukipenda kwa tamaa ya ngono ukishashibishwa nayo hutakuwa na sababu ya kumpenda mpenzi wako, matokeo yake utamwacha.Ukiwa umeamua kumpenda dada fulani kwa sababu anavutia, kumbuka kuwa anaweza kupata ajali akapoteza mvuto au akazeeka. Je umeshajiuliza swali itakuwaje kama mpenzi wako atapata makovu, utafanyaje baada ya mvuto wake wa usichana kuisha, nini kitafuata baada huyo mwanaume unayemsifia kwa tendo la ndoa atakapofikia ukomo wa kukutosheleza? Nadhani ni kuachana.
Sababu nyingine inayochangia wapenzi kuachana ni kutojali changuo sahihi kulingana na jinsi mtu mwenyewe alivyo.Mimi niliwahi kusoma katika Biblia Mungu akiweka wazi namna alivyozingatia kumuumbia mke Adamu kwa kusema, alimuumba mtu wa kufanana naye. Hivyo ni busara kupata mpenzi wa kufanana na wewe kwa tabia na mambo mengine ya msingi, bila hivyo mapenzi hayawezi kudumu.Kwa mfano kama wewe ni mtu wa imani kali, inakuwaje unakwenda kupendana na mpagani, huoni hicho kitakuwa kikwazo cha penzi lenu? Kwa msingi huo, lazima kupendana kuambatane na kufanana elimu, mtazamo na hata tamaduni, hii itasaidia kuondoa vikwazo vya mapenzi kuvunjika.
Lakini jambo jingine linalowafanya wapenzi wengi kuachana ni kutojali au kutofahamu kanuni za kutunza penzi. Kuna watu wanaweza kuchaguana kwa kuzingatia maelekezo yote, lakini wakajikuta wanaachana kwa kutojua namna ya kukuza na kudumisha upendo wao.
Nasema hivyo kwa sababu, kumpata mpenzi ni jambo jingine na kumtunza ni hatua nyingine ambayo ni ya msingi. Inawezekana kabisa ukampata wa kufanana naye, lakini ukajikuta unashindwa kudumu naye kwa sababu ya kumuudhi mara kwa mara tena kwa kusudi, kumnyanyasa, kusikiliza umbea, wivu, kutomjali na kumpuuza.Kinachosikitisha sana katika mapenzi ni kuona watu wanawapata wapenzi wa kweli, badala ya kufurahika nao wanawachezea kwa kufanya vurugu na kuwa waanzilishi wa usaliti na ujeuri. Ushauri wangu ni kuwa, ukipata wa kukupenda usimchezee, mtunze na umuonyeshe kweli kuwa wewe ni wa kufanana naye.
Mwisho, mapenzi lazima yakose sababu, ukiulizwa unampendea nini mpenzi wako? Jibu liwe sijui, kwani ukitaja sababu yoyote unakuwa katika hatari ya kuachana kwa vile kila sababu ina mwisho wake. Penzi ni lidhiko la moyo lisilokuwa na kwa nini. Ukisema nampenda kwa sababu ananijali, asipokujali, ukisema ni mzuri akiwa mbaya, ana pesa akiishiwa, mtundu,..uwanjani akichoka? Bila shaka penzi nalo litachoka!

Makaya's Forum: AMUA YAKO.
Makaya's Forum: AMUA YAKO.: Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa,akiamini kufika darasani ...
ONA MATATIZO YAKO MADOGO.
Nafahamu kwamba katika maisha ya kila siku hayakosekani mambo ya kuumiza. Sina
shaka kuugua, kufiwa, kukosa chakula, kusalitiwa katika mapenzi, kudhurumiwa,
kufilisika na kufutwa kazi ni mambo ambayo huzaa huzuni na machozi miongoni mwa
watu wengi. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba unalia au kuhuzunika kwa
sababu matatizo yako ni makubwa au umekosa kufahamu kanuni ya maisha aliyoitoa Mungu.Hebu jiulize ni wangapi wanahuzunikia mishahara midogo wanayolipwa makazini mwao, Je katika huzuni hizo ulishawahi kuwaza kwamba kuna binadamu
wengine hawana kazi na wanahangaika kutafuta shilingi mia tano kwa kuuza mihogo
na karanga kwenye kona za mitaa huku wakiwa juani?. Kama hao wapo ukubwa wa
tatizo la kukosa kazi unaokuliza kila siku uko wapi?
Uko wapi ukubwa wa tatizo la kutokuzaa
wakati kuna waliozaa na watoto wote wakafa. Kimsingi uwiano wa shida na
uhimili wake unaopatikana baina ya mtu na mtu, kamwe sifa ya huzuni hailetwi na
ukubwa wa tatizo, isipokuwa ni kukosekana kwa sanaa ya kuishi, yenye maono na
hisia za kupunguza mambo makubwa kuwa madogo.Katika hisia, mwanadamu hawezi
kuzuia machozi ya furaha au huzuni yasitoke, maana nilisoma katika Biblia kuwa
hata Yesu alilia pale alipopata habari kwamba rafiki yake Lazaro amekufa.
Lakini pamoja na kilio hicho hakusita kuita maono na kuona kwamba tatizo
lililokuwa mbele yake lilikuwa dogo, akaamua kuchukua hatua ya kuwaagiza
wanakijijini waliondoe jiwe na yeye kutajwa kumfufua kwa kutumia uwezo wake
(Haya ni ya kidini siyajadili sana katika mada hii).
Ifahamike kwamba kila mwanadamu ana uwezo wake wa kufanya, zaidi ya tatizo
analokutana nalo, lakini uwezo huo hauji kama sanaa ya maono na ‘udogoshaji’
matatizo haujapewa kipaumbele. Kuna watu wanalia kila siku kwa kuhitaji utajiri, lakini hawafikii
malengo kwa sababu wanaona umasikini ni jambo kubwa na kuufikia utajiri ni
jambo kubwa pia.Kwa mujibu wa utafiti wa William Frey mkemia na Mkurugenzi
wa Kituo cha Dry Eye and Tear Reseach cha Minneapolis, watu hulia katika
makundi matano tofauti ambayo ni: Wenye kujawa na huzuni zinazosababishwa na
matatizo ya kimaisha 49%.Wanaolia kwa furaha ni alisilimia 21, hasira 10% na
huruma 7%, huku wenye wasiwasi wakilia kwa kiwango cha asilimi 5 juu ya wenye
hofu wanaolia kwa asilimia 4.Lakini, pamoja na kuwepo kwa makundi hayo sita,
mwanadamu mwenyewe anatajwa kuwa na uwezo wa kuyabadili maono yake kwa kila
kundi na kupata matokeo tofauti kabisa, kwani hasira ikipunguzwa kwa kuona
kichocheo kilichojaza hasira ni kidogo pumzi hushuka na mtu hujiona mwenye
utulivu tofauti na mwanzo.
Vivyo hivyo, kwa anayelia kwa huzuni, huruma, wasiwasi na hofu,Kwa mantiki ile
ile hakuna haja ya kuhuzunika kwa kiwango cha juu, wakati kuna kiwango cha
chini cha kujiweka huru, nacho ni cha kutazama mambo makubwa kama madogo yasiyodumu na kwamba
saa, siku, miaka michache ijayo yatapita. Jiulize hapo ulipo msomaji wangu ni
kitu gani kinakuliza? Fahamu kwamba hulii au kuhuzunika kwa sababu matatizo ni
makubwa, bali umekosa ufahamu wa maono.Hebu chukua jukumu la kudharau shida
zako kwa kujilinganisha na wengine ambao bila shaka wanakuzidi matatizo. Fanya
hivyo kila unapokabiliwa na tatizo, usilione tatizo ni kubwa kwa takwimu,
lichukulie kuwa ni dogo kisha uanze kulishughulikia, utaona linamalizika kwa
ushindi mkubwa. Kamwe usijaribu kulitatua ndani ya maono yanayolikuza, hutapata
matokeo mazuri.Ukiwa ni umasikini uone ni mdogo, kututokuzaa, kukosa kazi,
kuteswa na mume na matatizo yote yatakayokukuta katika maisha yako yaone ni
madogo kisha tumia nguvu zako zote kuyakabili nina hakika utayashinda kirahisi.
Jaribu kupunguza matatizo, badala ya
kuyakuza kwa kuona hayawezekani kutatuliwa, utaona maajabu. Tambua kuwa tatizo lako si kubwa
bali unalikuza katika mawazo yako, kwa kuwa wapo wenye matatizo makubwa zaidi yao na hawalii
kama wewe.
Friday, November 23, 2012
Makaya's Forum: ONA KUSIKIA.
Makaya's Forum: ONA KUSIKIA.: Mapema ni kheri kuona bila ya kusikia,maana haya machache tumeyasikia hapa kwa kuwa yalionekana mwanzoni,jambo likiwa linaanza huonyesh...
Wednesday, November 21, 2012
MY LOVE FOR YOU...
More of my love for you, you
increase your pocessions and with how they can,
You make me, When you give me the courage which is suitable to be untold,
You water my flowers, my flowers grows through you,
You become the leader of the others and me too,
Indeed I will always love you,

Be with me more closely might
increase understandings, for us all...
What a man without anger whether not to do in front of me,
Its decently enough, it’s enough message, you do what’s enough for you to do,
Don’t just walking away and betray, someone is in hurry for the mean positions as it may portray, People want to own their own that’s in the future there should be no warning,

Do not let go more as ‘enough’ of satisfaction;
I am happy to love you, Try to rise up together;
try to be as well not at that moment only the designated to continue, to grow,
lets breath that was a tip…
Non even not our harsh, life giving
to the child is better than the child’s self, for other thing to be born to the
other thing, either you are blind, or indeed is that I should love you, maybe it’s
your time, You probably deserved to happen for the first time, the pain you
gave me is not a tiny, At when I try even to take the phone and call you, but
you’re not here again.
Then I would have even remember, I remember you my partner, to
remember our presence in peripheral, because often you made
me here, we have come regardless of things, Although you have the shield but
the courage to take my life also.Because of today's nature,
today is the day of your day , today has to complete that, For fathers, mothers,
brothers and sisters who have been together with me, Then I love YOU as my
words is within you.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
-
Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ...
-
Makaya's Forum: AMUA YAKO. : Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa...
-
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU. : YAFANYE MAPITO YAKO KUWA NGUVU INAYOKUSUKUMA KWENDA MBELE UKITEGEMEA KUISHI NDOTO ZAKO NA S...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa...
-
Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya...
-
Makaya's Forum: MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA.. : Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi,maana kwa kutokuyapenda na kujifanya ...
-
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...
-
Makaya's Forum: NIA NA THABITI YAKO MWENYEWE : Pengine tusije tukaenda madukani tukasema ni akili zetu,hii ikiwa kuna kuagizwa ama kwend...