Saturday, May 18, 2024
Makaya's Forum: ELEWA 2
Saturday, March 30, 2024
ELEWA 2
Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata
ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa kuelekezwa,kimfumo
kumtafuta mtu kwenye kundi ni ngumu,ili kutofautisha kama kuna mwizi,malaya au
mlevi ni kuangalia alipoiba aliekea wapi maana vyote vinaweza kuwa vya mtu
mmoja.
Sifa mbovu inayotembea ni sawa na rungu la kichwa ukiwa usingizini, katika miliki matendo mabovu yamekuwa yakitendeka bila woga kuliko mawazo ya mazuri,anayekusifia mazuri hadharani anakusubiri utoke,yule asiyekusifia ana ubaya wake mwingine wa kuelezea.ukigeuka watakwambia hawajakuita na hata wakikuita hawana cha kukwambia.
Kuna namna ipo umefanana na wazazi wako,hata isipokuwa sura basi hasira,tabia wengi wametokea utotoni usimlaumu mtu kwa kuwa malaya vile unavyojisikia kunywa pepsi mwingine coca,vingine vipo ndani ya damu hivyo tembo akinya sogea mbali pengine uchafu utakumwagikia alafu iabidi uelewe kufuata yako.
Kuna muda huelewi,yaani hata nilichokiandika hauelewi,tatizo lisije kwangu
maana ulivyovijaza kichwani mwako vyaweza kuwa kinzani na hivi,nikawa naandika
kwa kutumia wino mweupe.kuna mmoja alisema yanatoka popote bila kujua yametokea
wapi,ukitaka kupaa kuwa na mahusiano ya karibu na ndege.Usipojua yanatoka wapi
jaribu kuwaelewa ndege kwanza.
Watu ni zaidi ya chochote,yoyote yule umwonaye.hata sifa zangu hakuna nzuri
imekuwa kwa mwengine,maana kila mtu ananjia yake mafanikio sio utu,ukitaka pesa
watakutesa.unapotaka kunielewa isiwe kwa mlengo wako,mtu akitaka kukuelewa
asikuelewe anavyokuelewa Ukiishi usimwambie na mwenzio baadaye atajiita kuwa
mshauri.
ELEWA 1
Usidharau upendo unaoupata,sio kila kinalengwa kinalengeka,ukiona mchele umeota kwenye maji kuna ardhi chini ,haihitaji nguvu kupanda mbegu,itakuchosha mapema na utapoteza furaha yako vivo hivyo,asikwambie mtu kucheka wakati mrefu wa kununa ni nguvu tosha na ikakupa amani muda wote.
kama hakuna jibu kwanini uliingia kwenye mdomo wa mamba basi
utakuwa unaishi nao,kujua kuogelea sio kuitii kiu ya maji ya kunywa,sehemu nyingine
za kuogelea kuna mamba,wazee hupendelea sana swimming pool,sehemu za kuogelea
ndogo ,vijana hujitupa maziwani na mabaharini na wakifika katikati hushituka na
kujilaumu,na huo huwa msingi wa kubomoka.
Kuna maziwa na bahari nyingine zina ghasia sana,utaratibu
mtu mmoja lakini wao huwapanga hata ishirini,mawimbi yanatoka popote kwenye mwelekeo,bora swiming pool mawimbi
utayaleta wewe.wanasema saidia uendelee na safari,ni vile unatoa dhaka na mchungaji anaenda kununua shamba ili
alime apate chakula cha kuuza na familia.
Elewa kwamba sio yote unayoyaona lazima uyaelewe,hata kama umeyasoma
sio lazima uyaelewe,elewa wengine wa kuwaacha,kataza moyo wako kushikamana na
matendo,Elewa duniani kuna watu watataka kwa lazima kufikiria tofauti ya wewe
unavyofikiri ili wao kuonekana tofauti.
Wednesday, January 24, 2024
Makaya's Forum: ISHI NA YAKO
Makaya's Forum: HASIRA YAKO
Tuesday, January 16, 2024
HASIRA YAKO
Unakasirikia maisha yako wengine wakiwa na furaha,ikiwa lengo si kutaka kuijua furaha ya mwengine bali kujua ni namna gani hasira zako zinakupeleka,binadamu tupo tofuti,mmoja hali nyama ya mbuzi kwa kuwa inamtoa vipele mwengine hali nyama ya nguruwe kwa sababu ya dini sasa nikikasirika usiniulize nimekasikia nini,nina mengi.
Kasirika,usikarike pasipo na
sababu.upumbavu wa mtu mmoja usikufanye uvunje simu na mwengine kufikia kumkata
mtu panga.angalia unapokasirika sauti yako ya ndani inakwambia nini na kabla
haujatenda kwa kutumia kiungo chochote cha mwili yakupasa kutafakari,maana kuna
wale wenye hasira za ndani(chuki) hawafanyi mambo yao hadharani.
kama ilivyo katika michezo
mmoja akamchezea rafu mwenzake basi wanamichezo waliiga kwenye maisha,na ndiyo
maana unasikia michezo haiitaji hasira,ukisusa wenzako wanakula na wenzako huwa
wanakula mpaka baadaye ukakitamani tena hicho chakula,kasirika vizuri.
Dunia hadaa utakasirishwa
wakitaka kujua maamuzi yako,ukishajua umekasirikia nini maamuzi yako yawe
tofauti na hasira zako kwani kweli maisha yana mengi lakini kuna mengine sio ya
kukasirikia fikiri mtu anakasirikia mafanikio yako na atayekumbatia maamuzi ya
hasira zako yampasa kuwa yeye.
ISHI NA YAKO
Watakwambia unabahati kwakile ulichokifanya kilichokufanya uwepo hapo,kujipa ufalme na kuzungumzia maisha ya mwengine kwa kuwa umefika mahala fulani,tambua maisha yana stepu,uliyopo sasa mwengine alipita juzi ukicheka leo mwenzako kulia ni sawa na kulia wakati mwenzako anacheka.
Usibabaike na waliowahi
kufikia ukitakacho,tambua muda wako ikiwa unajiandaa jiandae vyema ili ukikosa
isiwe lawama kwa wengine,maana imekuwa mmoja akishindwa akatoa sababu za
mwengine kumuangusha.
Usifikiri ni raisi kukaza
jambo,kuna mengine yanakaza mpaka kufungua inakuwa kama ni kukaza,ujiandae
vyema maana kuna vilio,maumivu yasiyo na machozi na hata usumbufu
usiohitajika.yatambue magumu yako na jipe muda kuyatatua ikiwa humu duniani
wote mpaka muda huu tunatafuta maisha.
Kheri udongo unarudi utokapo
maana ingekuwa foleni kubwa barabarani kwa kuwapa heshima wajionao
miungu,usifikiri wakati wa magumu peke yake mwishowe ukawapa lawama watu wasio
husika na maisha yako,tambua nafasi yako si ile aisemeayo mwengine,watu huwa wanaongezea
kwa kile ulichonacho.
Monday, October 9, 2023
Makaya's Forum: NAONA
NAONA
Naona umekalia mguu wako ukijaribu kutupa mkono kulia ili usaidie kusimama na mguu wa kushoto,naona ukiambiwa acha kwa kuwa hujajua kuwa ni moto na unaunguza,Naona vingi ukipata uelewa ntakuelewesha.
Naona wamefunga milango wakijua upo nje,wamefunga njia ikiwa bado haujapita,wanakusema unakonda kwa kukataa kunywa uji,naona ukisoma herufi bila ya kuelewa,umeanza kuita mma ukijua ni uhai,naona chuki juu ya moyo mkunjufu,Subiri ukipata uelewa ntakuelewesha.
Naona hujajua kama sufuria sio kikombe,hujajua mtu anayesubiria hakupata hajapata sifuri,usikimbilie kuendesha vitakavyo kuendesha,subiria kupandishwa basi likisimama utashushwa,Unapokula usijichafue sana meza wapo wabaya watu wanaotafuna vya kumeza.
Naona unaanza kuelewa ya msingi,ukitaka kujisaidia waogope watu na isiwe kwa chuki ,kama umekuwa jua safari unaiweza na unapoelekea naona safari ndo inaanza,Naona unashindwa kufanikiwa kwa fitina nyingi,vita zipo nyingi kaa mbali na maadaui,binadamu yoyote anaweza kuwa adui bila hata wewe kutaka,naona unakuwa msuruhishi mbele ya ndugu zako na sio kuwagandamiza.
Kesho naiona tena,naliyaona ya jana yakanipa majibu ya kuwa mtihani ni ule ule.naona yake akae nayo yako baki nayo mwenyewe ili kutokuchanyikikika,Naona unakanyaga maji na hakuna sehemu yenye moto ,Naona nisikuchoshe Sali sana kaa mbali sana na ndugu msumali.
Thursday, October 5, 2023
NEEMA YA MUNGU
Neema ya Mungu haipangwi na mwanadamu ,maana siwezi kuomba na kutaka nijibiwe kesho ama muda ule nitakaotaka ikiwa naamini Mungu anapenda maisha yangu na yupo bize kuhakikisha shetani hanichukui moja kwa moja,
Ufahari na mafanikio unaweza kuwa hitaji la kila mmoja lakini vitu hivyo vinagharama na unaweza kulazimisha kugharamia ukawa navyo lakini ukakosa namna ya kuendesha na kufurahia uliyochonacho,ikawe muomba jiwe akapewa mkate.
Namshukuru Mungu hata nisingekuwa hapa,naishi vile Mungu ametaka na ifike kipindi nisisahau wala kudharau kusali na kumwomba kwa kuwa yeye ananipenda,anabadili kile kitu kinachosumbua nafsi yangu ,anajua ninachohitaji na muda wa kunipa.
Najua maisha yangu hayajabadilika hivi hivi bila neema ya Mungu,pale ninapo muomba ananipa,anabadilisha mazingira.Hata kesho sitasimama peke yangu maana ndiyo umenifikisha hapa nilipo,
Maombi mengine ukatizwa na hofu na kuzuia neema zisikudondokee,namuomba Mungu nifanye tofauti na hofu ilivyo iwe kutaka,kuendea na kukipata kukiwa na maono juu ya kile ninachokihitaji,
Ndoto hata ikifeli moja ntaota tena maana neema yako Mungu haina muda kamili,muda wa kupata kitu zaidi kile mtu usichokidhania.
Wednesday, May 27, 2020
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU.
Tuesday, April 23, 2019
Makaya's Forum: KATAA
Saturday, April 20, 2019
BINADAMU UNAPOJIULIZA(usimwachie Ulimwengu)
Najiuliza umeniuliza kwanini Sitoi salamu nami huwa najiuliza pia kama huwa unaipata salamu yangu,ikiwa ubongo wa mwanadamu wa kila aliyeumbwa una swali la kujiuliza jiulize unaelekea wapi maana kila siku zinavyokwenda ulimwengu unaelekea na kuzidi kutoa maswali yanayoendana na technolojia ambayo haikukupa misingi yenye mizizi ya kina katika kujua mambo yaliyo duniani yanayoendana na maswali hayo katika kukabiliana na maisha ulimwenguni.
Nimekuja kuishi duniani hivyo nina kila sababu ya kufanya hivyo iliyo vyovyote ili iwe, niishi. kutangulia sio kufika lakini sio katika kifo na hii mara nyingi hunipelekea kujiuliza naishije ama ntaishije ? sasa hili ni chaguzi ukizingatia Moyo nao hutaka kuamua yake pindi majibu yanapotoka hivyo bila kuuhusisha moyo wangu huwa nayavumilia majuto ikiwa pia nazingatia na muda nilioanza kupata wajukuu na kusoma hali zaidi kupitia hapo,
Maisha yana mengi ni mtihani hivyo maswali mengine siyo yako ukiyajibu unakuwa kama unatumia akili yako vibaya,Kama utapenda kuyajibu na kuona umepata zaidi basi Mwalimu(Ulimwengu) ndiye atakayesema kweli kuzingatia na muda na ujue binadamu ameumbwa kupambana kila siku,
Friday, April 19, 2019
UNAPOWAZA
Sikuwaza umri ni kama haya makubwa ninayoyawaza,wala kuna mengine sijawaza lakini yamekuja katika haya,mawazo ukiyaamini,yanakuletea imani yako inachokiwaza hata ukajiandae na utofauti ili kutokuyazidisha yaliyopo,maana nawaza sikufika hapa kama nilivyo wala sikuwa mimi kama nilivyo,sio tu kwa sababu ya nini ama fulani nikiwaza kwa mawazo yangu ni imani maana sikuijua kesho zaidi ya yule aliyeniambia niache kufanya ya kesho kwa kuwa hata usiku wa leo hayajafanyika.
Nawaza ni kheri nizeeke muda mwingine ntakuwa nimepita mengi,nisionekane tu kwa mtu anayeona aonavyo bali nikajifiche kwa vile waonavyo,nilikaa na kuanza kuandika haya nliwaza mmoja atawaza yale ni mawazo tu,lakini kwa jinsi navyoona hata yule asemaye naye anataka kuonekana na mawazo bora,kuna vitu Mwenyezi Mungu amekupa na mwengine hana,Kama unaweza kufanya chochote bora fanya katika ubora uwazavyo.
KATAA
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofauti na vile inavyoweza kusukumika,upepo unaweza vuma kuelekea kusini na yenyewe maisha yakataka uelekeo wa magharibi itakuwa na kueleweka vile inavyoonekana uelekeo ulivyo.
Muda mwingine unaweza kudhani hata ulikosea kufanya kile unachokifanya au ulikosea kuoa,ulikosea kununua mashine fulani hata pengine ulikosea kumwambia mtu fulani jambo fulani na mengine mengi.Kile kinachosukuma mwelekeo kinatagemea uwiano wako na ukikataa kwenda kulia na msukumaji anasukuma kushoto basi jua utaenda kushoto tu.
Sunday, March 24, 2019
Makaya's Forum: BADILIKA.
Friday, November 18, 2016
SHIKA YAKO
Watu wanaona wanachowaza wao juu ya wenzao ni sahihi zaidi, yaani mtu anaamua kumwamulia mwengine kwakuwa tu labda wametofautiana katika hali zao hasa katika uchumi wa binafsi na pengine ikawe ni tabia na kujifanya nafsi ya mtu iko mikononi mwao.
Sibishani na mtu ili akapata faida,aliyetaka kuelewa aliuliza mapema kile kinachohitajika kufanyika na kikafanyika , hakuna haja ya kulazimisha kujulikana kama unajua na wakati haujui, anayefanya jambo moja huacha kutokana na mtu mwengine karibu kufanya jambo lile lile, na aliyeamua kufanya jambo hakatazwi kwa maneno ama kwa kile kilichofanywa,na akiacha isiwe kwa maneno maana kuna binadamu wanajua ya wenzao kuliko wenzao,wakijiweka wao bora zaidi ama tu kukuchafua kwa vile mpumbavu hachagui neno la kukusemea,
Tuesday, October 11, 2016
KUZA KIPAWA CHAKO NA KATAA KUSHINDWA.
Tuesday, September 27, 2016
YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU.
Yafanye
mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako
na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyiyale wanayoyategemea zaidi
ya kile kilichopo pasipo kufikiri ni kwanini mtu anajawa na msongo wa mawazo yanayokataza
kuishi ndoto zako.
Labda
kwa sababu ya watu na matendo yaliyopita yanaisumbua roho yako, watu
wengi wanaishi wakikimbilia wasichokijua kwa kuogopa nafsi zao kubaki nyuma na
baada ya kuangalia wanajikuta walichokifanya kilipaswa kufikirika kabla ya maamuzi
ya kutenda, hivyo kukuletea shida katika kufanikisha mambo pasipo kujua
wapi walianza.
Wengine wanaishi maisha yao kwa kujiona, kujiona kwamba ndiye yeye,ukijiona kwamba u tajiri na wakati bado ukihitaji msaada na kuuacha uhalisia, kwamba kila kitu kipo sawa katika malengo na yale unayoyahitaji huku unasahau maisha yanakutegemea wewe, kwa lolote unalolitafuta na lenyewe linakutafuta, ni kama nguvu ya mvutano.
Hivyo ni lazima kuwa nalo jambo, acha kufanya lile lisilo na tamanio kwako na fanya kile unachoweza maana na chenyewe kitafanana nawe, ukitembea sana katika maisha utakutana na kauli ambazo nyingine zinasimamisha na kurudisha nyuma nafsi yako, ikiwa lakini yako utaitumia vizuri ukiangalia ni wapi utawekeza akili yako na baadaye uyaache maamuzi yako yakikufata sambamba nawe.
Angalia katika njia ambayo unaweza
kuyatengeza maisha yako yakawa vile utakavyo kama vile ukaamini kwamba ipo siku maisha
yako yatakaa na kubadilika ukiamini unaweza kuyafanya maisha yako katika
yale utakayo yakakurudia ama kukupata upya, kama hauna kitu nyanyuka na ukafuate
kile unachokitaka.
Hutapoteza kile unachokitaka kipo na kinakusubiri wewe kama bado ulikuwa haujakipata,achana na mawazo ya kilichopotea maana unapoelekea ni mbele kupata maana amua sasa ili watu wengine waje wasome kupitia wewe.wengine wanasema hapana huku wakiwa hawajui kama wanakataa juu ya nini.
Nguvu iliyopo ndani yako ni kubwa,jiamini na safiri na nyota yako.
Sunday, September 25, 2016
FANYA LEO YAKO
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
POPURAL POSTS
-
Unapokwenda ni sawa,kwa kuwa kila siku kadri ya zinavyokwenda mwanadamu anaishi katika ile hali ya kutokusema kwamba!! na sio haielewe...
-
Hata usipozungumzia utaifa lakini kiwango cha maisha ya mtanzania ni kidogo sana,hapa nikiwa nazungumza na watanzania wale walio na nd...
-
WALTER CHILAMBO SPEECHWISE.. NI mshiriki wa EPIC BONGO STAR SEARCH ANAYETOKEA MBEYA,HIVI SASA AKIWA KATIKA FAINALI HIYO ITAKAYO FANYIKA DI...
-
Kufika sio kuwahi yaweza kuwa kuwapo ama kutangulia,na yale yanayotokea sio lazima kupanga kwani mara nyingi tunasema hatupangi sisi za...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Kufikiri ni kuwa na hitaji la kurekebisha jambo,kunatokana na mawazo,kwa hiyo fikra zinaweza kuwa ni mawazo,kufikiri ni kitendo,kure...
-
Ni namna ya maisha yanavyokwenda,maana leo ikaja lakini siyo kesho,ukawa na hofu ya leo maana ile ya jana nusu imeishia leo.. kama i...
-
Unakasirikia maisha yako wengine wakiwa na furaha,ikiwa lengo si kutaka kuijua furaha ya mwengine bali kujua ni namna gani hasira zako zinak...
-
Watakwambia unabahati kwakile ulichokifanya kilichokufanya uwepo hapo,kujipa ufalme na kuzungumzia maisha ya mwengine kwa kuwa umefika mahal...
-
For all those who stand and see, as where the sun rise and shine, It is not to stay and think alot that life is going too hard I do no...